Sagini Aendelea Kuboresha Miundombinu Shule ya Awali na Msingi Mwalimu Nyerere

GEORGE MARATO TV
0


Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini ameendelea kuboresha miundombinu ya Shule ya Awali na Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo Kijiji cha Butiama ili kuepukana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo watumishi na wanafunzi ikiwemo wizi wa vifaa vya kujifunzia.

Akizungumza katika Mahafali ya Tano ya Darasa la Saba yaliyofanyika Agosti 22, mwaka huu Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini, Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Emmanuel Mayeji aliyemwakilisha Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa Mhe Sagini alianza kutatua kero hiyo mapema na sasa ni zoezi la ukamilishaji wa ujenzi wa uzio wa shule.

"Mhe. Sagini amewaahidi kwamba atakuwa nanyi bega kwa bega katika kukuza elimu wilayani  Butiama kwani ni maelekezo ya Chama cha Mapinduzi kupitia Ilani ya Uchaguzi wa mwaka 2020 – 2025 iliyolenga kuimarisha ubora wa elimu katika ngazi zote kwa kuzingatia falsafa ya kujitegemea yenye kuendana na mazingira ya nchi yetu," amesema Mayeji.

Aidha Ndg. Mayeji amefarijika na kuwapongeza Viongozi, walimu na wanafunzi baada ya kuisoma Risala ya Mkuu wa Shule hasa katika kipengele cha mafanikio ya kitaaluma. "Nimegundua tangu shule hii imeanza haijawahi kushuka wastani wake wa ufaulu wa mitihani ya Taifa ya darasa la saba.

Mwaka 2021 Shule ilipata wastani wa 255.5714.,

Mwaka 2022 Shule ilipata wastani wa 264.7059

Mwaka 2023 Shule ilipata wastani wa 280.9615.

Mwaka 2024 Shule ilipata Wastani wa 287.2500."

Hata hivyo katika Hotuba ya Mhe. Sagini iliyosomwa na Ndg. Mayeji ilieleza kuwa  juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kujenga madarasa 15,000 kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19 jinsi zilivyochagiza ongezeko la udahili katika shule za sekondari hivyo kuna kila sababu ya kumshukuru Mhe. Rais kwa kuwa wahitimu  wa 19 wa Shule ya Awali na Msingi Mwalimu Nyerere na katika shule nyingine wilayani Butiama watakuwa na uhakika wa kujiunga na Shule za Sekondari zilizojengwa na Mhe. Rais.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top