Mama mzazi wa Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akimpa baraka mwanaye muda mfupi kabla ya mgombea huyo mwenza kwenda kuungana na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan, kuchukua fomu za kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu leo, tarehe 9 Agosti 2025, katika Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.



Comments
Post a Comment