MwanaFA arejesha fomu INEC, asema mwaka huu CCM itafanya kampeni bab'kubwa

GEORGE MARATO TV
0


MGOMBEA Ubunge Jimbo la Muheza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA, jana amerejesha fomu yake ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi Jimbo hilo na kusema mwaka huu chama hicho kitafanya kampeni ili kusaka kura nyingi za mgombea Urais wa Chama hicho Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu yake kwa msimamizi wa Jimbo Serapion Bashange, alisema kuwa amehitimisha zoezi la kuchukua fomu ya kuomba uteuzi wa tume hiyo lakini amewashukuru Wana-CCM wa Muheza kwa kumuunga mkono miaka mitano iliyopita lakini pia Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kwa kumteua tena kuwa mgombea wa Chama hicho katika Jimbo hilo.

"Nawashukuru Wana-Muheza kwa kuniunga mkono miaka mitano iliyopita tumefanya mambo makubwa ya maendeleo, imani mlionipa kwa kunichagua kwa asilimia 91 ni deni kubwa ambalo nawahakikishia ninakwenda kulilipa kwa vitendo baada ya uchaguzi Mkuu Oktoba 29,"  alisema.

MwanaFA amemaliza ubunge akiwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, alisema kuwa miaka mitano amefanya kazi na Wana-Muheza ilikuwa ni mwanzo mzuri lakini sasa kupitia Ilani ya CCM ya mwaka 2025-30, anakwenda kufanya makubwa kutekeleza miradi mingine ya maendeleo.

Aliishukuru Kamati Kuu kwa kujenga imani naye kumpa nafasi nyingine ya kupeperusha bendera ya chama hivyo pamoja na viongozi na wana-CCM wanakwenda kutafuta kura za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili wilaya hiyo iongoze kwa kura kati ya majimbo 12 yaliopo mkoa wa Tanga.

Akizungumza namna watakavyoendesha kampeni za CCM mara baada ya kuzinduliwa na Rais pale Kawe Jijini Dar es salaam, MwanaFA alisema watafanya kampeni ambazo zitakuwa na matamasha ya muziki ili kutoa burudani lakini pia kukuza vipaji vya wasanii wilayani hapa.

Awali Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Simon Leng'ese aliwashukuru Wana Muheza kwa kujitokeza kwa wingi kumsindikiza mgombea wao akisema CCM ilikuwa ikijaribu mitambo yake kabla ya kuanza kampeni zenyewe.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top