Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

GEL yatoa fursa za udahili wa papo kwa papo maonesho ya Dar


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Global Education Link (GEL) imewataka wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu kuwa makini na kozi wanazochagua wanapotaka kujiunga na vyyuo vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Ushauri huo ulitolewa jana  na Meneja Mkuu wa GEL, Regina Lema, wakati wa  maonesho ya kitaaluma ya vyuo vikuu mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za sekondari zaidi ya 102 za Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema GEL imekuwa ikitoa mwongozo kwa wanafunzi mbalimbali kuhusu kozi sahihi wanazopaswa kuchukua wanapokwenda kusoma vyuo vikuu mbalimbali na kwenye maonesho hayo wametoa elimu hiyo.

Regina alisema mbali na kutoa elimu hiyo, GEL imetoa huduma za udahili wa papo kwa papo, pamoja na ushauri wa taaluma na malezi ya kitaaluma kuwawezesha wanafunzi kuelewa vyema nini cha kusomea kwa ajili ya kufanikisha malengo ya Taifa ya mwaka 2025 hadi 2050.

Regina  alisema kuwa kupitia ushiriki huo, GEL pia limeimarisha uhusiano wake na shule za msingi na sekondari kwa kushirikiana na walimu na wanafunzi waliotembelea mabanda yake.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Albert Msando, alisema kuna umuhimu wa wanafunzi wakawekewa mazingira rafiki ya kuwa wabunifu na kufikiri ili hatimaye taifa liwe na kizazi chenye uwezo wa kufikiria kufanya mambo makubwa.

Maonesho hayo yaliyoandaliwa na Global Education Link (GEL), yanaendelea kwenye viwanja vya Mlimani City jijini ambapo maelfu ya wanafunzi wa shule za Dar es Salaam zinashiriki kupata mwongozo wa kusoma vyuo vikuu.

Msando alizipongeza taasisi zote zilizoshiriki kwenye maonesho hayo na kuongeza kuwa kuna umuhimu wa shule na taasisi za elimu kuonesha  thamani ya elimu wanayotoa kwa vizazi vya sasa na vya baadae. 

“Tusipokuwa na kizazi chenye elimu bora tutaendelea kusubiri sana, tukiwa na kizazi kisichokuwa bunifu tutabaki vile vile miaka nenda miaka rudi, tukiwa na kizazi kisichojua kufikiria tutaendelea kuwa watazamaji wakati wenzetu wanasonga mbele,” alisisitiza

“Elimu bora siyo anasa ni haki ya watoto nani wajibu wa watoa huduma ya elimu kutoa elimu bora na nimefurahi kuona watoto wadogo wanazungumza kichina hapa.

“Mimi sijui kichina lakini nimeona hapa watoto wanazungumza kichina kwa hiyo watanisaidia hata mimi siku nikipata wawekezaji wachina watakuwa wananitafsiria kwasababu bila hivyo wanaweza kuwa wanakusema wewe hujui,” alisema

“Hili ni jambo muhimu sana mmefanya ingawa  eneo kama hili gharama ni kubwa kufanya maonesho kama haya  lakini mkiandaa siku nyingine mtashirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo na nitatoa maelekezo mpewe eneo bure la serikali kama Leaders Club na Tanganyika Packers,” alisema

Msando alisema kwenye mabanda aliyotembelea, amefurahia kuona vijana wakifanya vitu mbalimbali vya kitaaluma ambavyo vinaonyesha ni kwa kiasi gani vijana hao wanavipaji na wanaweza kufanya mambo  makubwa kwa maendeleo ya taifa kama watalelewa vyema.

“Watoto wetu wanafundishwa kufikiria kwa hiyo wazazi na walimu lazima tuwasaidie tupate kizazi kinachofikiria. Taasisi za elimu ambazo nimeziona leo zinafanyakazi kubwa zinawaandaa watoto wetu kuweza kufikiria na kujiamini nawapongeza sana,” alisema

“Nimeona taasisi nyingi ikiwemo Global Education Link tujitahidi tufikishe huduma hizi kwenye ngazi za chini kabisa, kuna vijana wanaakili nyingi sana lakini wazazi wao hawajui watoto wao watasoma wapi, tutoke kwenye maorofa twende hadi ngazi ya mtaa tukawape maarifa ya wapi kwa kusoma,” alisema

Alizitaka taasisi za fedha kuingia makubaliano na wamiliki wa shule kuwapa mikopo nafuu kwaajili ya kuendesha shughuli zao za kila siku pale wazazi wanaochelewa kulipa ada kutokana na sababu mbalimbali.

“Kuna wakati mzazi anachelewa kulipa ada kutona na sababu mbalimbali kwa hiyo ili mwenye shule aweze kulipa mishahara ya wafanyakazi na gharama zingine za uendeshaji lazima apate mkopo nafuu kutoka kwenye benki ili kurahisisha shughuli zake za uendeshaji za kila siku,” alisema

“Shule binafsi zinaisaidia sana serikali hawa wote mnaowaona wanasoma shule binafsi zisingekuwepo hizi shule inamaana hawa wote wangekuwa kwenye shule za serikali kwa hiyo sekta binafsi inaisaidia serikali kwenye ukuaji wa elimu na utoaji wa huduma,” alisema Msando

Meneja Mkuu wa Global Education Link (GEL) Regina Lema,  alisema maonesho yamekuwa na mafanikio makubwa sana kwani wanafunzi wengi wamehudhuria na wengine wamepata udahili wa papo kwa papo.

Alisema wamefanikiwa kuwapa mwongozo wa kozi za vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi wanafunzi wa shule zaidi ya 102 waliohudhuria. 

“Namshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kufika kwenye maonesho haya na kwa kutupa fursa  ya kwenda kufanya maonesho kama haya mashuleni na tutaenda wilaya zingine za Dar es Salaam na mikoa mingine pia,” alisema

Regina alisema Global Education Link imekuwa ikipita kwenye shule mbalimbali kutoa mwongozo kwa wanafunzi kufahamu kozi zinazopatikana kwenye vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi na ufadhili unaotolewa na vyuo hivyo kupitia GEL.

“Pia katika maonesho haya tumefanya udahili wa papo kwa papo na pia hapa katika maonesho haya  tunawawakilishi wa vyuo vikuu vya nje ya nchi kwenye mabanda yetu na tunatoa huduma zote ambazo ungezipata ofisini kwetu na kwenye ofisi zetu ambazo zimesambaa nchi nzima,” alisema. 

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...