Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Agizo La Dkt.Biteko La Minada Yote Nchini Kutumia Nishati Safi ya Kupikia Laanza Kutekelezwa


📌 Wachoma nyama na Mama Lishe katika mnada wa Msalato Dodoma waanza kuonja matunda ya Nishati Safi ya Kupikia

📌 Dkt. Biteko asema ni matunda ya Rais, Dkt. Samia ambaye anayefahamu machungu ya kutumia Nishati isiyo safi ya Kupikia

📌 Atoa maagizo kwa Mkurugenzi Jiji la Dodoma kuweka miundombinu itakayohakikisha majiko ya Nishati Safi ya Kupikia ya Wachoma nyama yanakuwa salama

📌 Apongeza REA, Wizara ya Nishati kutekeleza agizo alilolitoa: STAMICO yatakiwa kuweka kituo cha kudumu cha mkaa mbadala Mnada wa Msalato

📌 Kituo kikubwa cha kusambaza umeme na kusimamia gridi ya Taifa kujengwa Dodoma


Agizo la Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko alilolitoa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha kuwa minada yote nchini inakuwa na miundombinu itakayowawezesha Wachoma nyama, Mama Lishe na Baba Lishe kutumia nishati Safi ya Kupikia limeanza kufanyiwa kazi ikiwa ni utekelezaji wa ajenda ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wote wanatumia Nishati iliyosafi ya kupikia.

Safari hiyo ya kuhakikisha minada yote nchini inatumia nishati safi ya kupikia, imeanzia katika Mnada wa Msalato jijini Dodoma ambapo tarehe 21 Agosti 2025, Dkt. Biteko amegawa majiko banifu kwa Mamalishe takriban 27 wanaohudumu katika mnada huo pamoja na majiko ya kuchomea nyama.

“Kama mnavyofahamu, Mhe. Rais alitoa maelekezo kuwa watanzania asilimia 80 ifikapo 2034 watumie nishati safi ya kupikia, maelekezo yake yanaendelea kutekelezwa, tulianza na taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100  kuondoa matumizi ya kuni na mkaa ikiwemo  magereza yote nchini, shule za Sekondari , vyuo na taasisi nyinginezo lakini moja ya maeneo yaliyobaki ni pamoja na minada ambayo inahudumia watu wengi.” Amesema Dkt.Biteko

Dkt. Biteko ameeleza kuwa kazi ya kufunga mifumo ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye minada ilianza na utafiti ili kupata hali halisi ya matumizi ya nishati hiyo ambapo katika utafiti huo, asilimia 89.5 ya wachoma nyama wote walisema hawana uelewa wowote kuhusu nishati safi ya kupikia, pia utafiti huo umeonesha asilimia 26.3 ya wachoma nyama wamewahi kutumia nishati safi ya kupikia na asilimia iliyobaki haijawahi kutumia. Hii ikionesha kuwa bado kuna kazi ya kufanya kuelekea kwenye matumizi ya Nishati Safi ya kupikia.

Amesisitiza kuwa, hatua hizo zinazochukuliwa na Serikali katika  Nishati Safi ya Kupikia, ni matunda ya Mhe. Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye amejipambanua kama kama kiongozi mwanamke anayejua machungu ya matumizi ya nishati isiyo safi na wakati wote anaelekeza kuwa yeye anachotaka kuona  ni watu wengi hawatumii nishati isiyo safi ya kupikia. 

Ameongeza kuwa, Tanzania ndiyo nchi pekee barani Afrika ambayo imezindua Mkakati wa Taifa wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambao umekuwa ni mfano barani Afrika na nchi nyingine zinakuja kujifunza hivyo lazima iwe mfano na kinara  kwa kuishi yale inayoyasema.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuweka miundombinu ambayo itafanya majiko ya nishati safi ya kupikia katika minada  mkoani Dodoma kuwa katika sehemu ya kudumu na zoezi hilo lianze mara moja.

Aidha, ameliagiza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuweka kituo cha kudumu cha kuuza mkaa mbadala katika mnada wa Msalato ili wananchi wasikwame pale wanapohitaji nishati hiyo.

Vilevile ameitaka REA, kuhakikisha majiko makubwa ya kuchomea nyama ambayo yanatumia Nishati Safi ya Kupikia yanapatikana ili wananchi wanaochoma nyama na wanaofuata huduma wasipoate madhara ya afya kuanzia sasa kwenda mbele.

Dkt. Biteko ameipongeza REA na Watendaji wa Wizara ya Nishati  kwa kupoeka agizo lake kwa haraka na kulifanyia kazi, pia amewaasa kuendelea na ubunifu utakaowawezesha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia na wasisahau kufanya tathmini ya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika minada hiyo.

Pia, amewaasa Mama lishe na Baba lishe kuiunga mkono ajenda ta nishati safi ya kupikia na kuwa mabalozi wa nishati hiyo kwani watu wakiona faida zinazotokana na kutumia nishati safi ya kupikia  kutoka kwao nao watavutika kuitumia. 

katika hafla hiyo,  Dkt. Biteko amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kubwa ya mfano katika sekta ya Nishati ambapo amesema Mkoa wa Dodoma  muda si mrefu utakuwa ni kitovu cha usambazaji umeme katika mikoa mbalimbali ikiwemo Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Arusha na  pia kitajengwa  kituo kikubwa cha kusambaza umeme na kusimamia gridi ya Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule kwa upande wake amesema walaji katika mnada wa Msalato  kwa wiki ni kati ya 2000 na 3000 hivyo kwa kutumia Nishati Safi ya Kupikia itawezesha kuokoa mazingira kwa kuondokana na kuni na mkaa ambao ulikuwa ukitumika kuhudumia idadi hiyo ya watu. 

Aidha ameomba a kampeni hiyo ya Nishati Safi ya Kupikia ifike kwenye masoko mbalimbali ambayo ina mama lishe na baba lishe.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba yeye amemshukuru Dkt. Biteko kwa maono yake ambayo yamewezesha Mnada wa Msalato kufikiwa na Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni mwanzo wa kusogeza huduma kwenye minada mingine.

Ameeleza kuwa kiwango cha matumizi ya nishati safi ya kupikia kimepanda kutoka asilimia 6.9  ya mwaka 2022 na hadi kufikia asilimia 20.3 na kusema kuwa kwa jinsi matumizi ya nishatil safi ya kupikia yanavyoongezeka Serikali itatimiza lengo lake ya kufikisha Nishati Safi ya Kupikia kwa watanzania wapatao asilimia 80 kama alivyoagiza Mhe.Rais.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema amesema katika mnada wa Msalato kuna wachoma nyama kati ya 45 na 50 ambao watapatiwa majiko makubwa ya kuchomea nyama, pia kuna mama lishe 27  ambao tayari wote wamepatiwa majiko banifu.

Mwenyekiti wa Wachoma nyama katika Mnada wa Msalato, Mathias Raphael  amesema baada ya kupata elimu ya nishati safi ya kupikia katika mnada huo  ameanza kutumia jiko linalotumia mkaa mbadala ambao amesema kuwa unatumika kidogo huku ukichoma nyama nyingi, unakaa muda mrefu na hauna moshi.





Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...