Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kampuni ya CRCEG inatekeleza kwa ubora na kasi ujenzi uwanja wa AFCON Arusha-Serikali


Na Prosper Makene, Arusha

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Hamis Mwinjuma ameipongeza Kampuni ya CRCEG ya kutoka nchini China ambayo inajenga uwanja wa mpira wa miguu jijini Arusha utakaotumika kwa michuano ya AFCON 2027 kwa kuweza kujenga uwanja huo kwa kasi na viwango vya hali ya juu.

Akizungunza mwishoni mwa wiki wakati wa halfa ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa zege na kuanza ramsi kufunga paa la uwanja huo, Naibu Waziri amesema kuwa ni mara ya kwanza nchini kuona mkandarasi anamaliza kazi aliyopewa kabla ya muda kwani amemaliza awamu ya kwanza siku 20 kabla ya  muda uliopangwa kwenye mkataba.

Mwinjuma alimaalufu kama Mwana Fa amesema: "Mkataba huu wa ujenzi wa uwanja mkubwa wa michezi jijini Arusha, ulitiwa saini tarehe 19, mwezi wa 3, mwaka jana (2024), lakini natambua kazi rasmi zilianza tarehe 25, mwezi wa 7, mwaka huo huo, baada ya utaratibu wa kukabidhiana site pamoja na shughuli zingine za awali kukamilika. Mkandarasi amepewa jukumu la kufanya usanifu, kujenga, na kufanya manunuzi muhimu yatakayokamilisha usanifu wa mradi huu kwa kuzingatia vigezo elekezi." 

Aliongezea, "Hivyo, tangu mradi kuanza, mkandarasi ulijielekeza kuanza kazi zako katika maeneo hayo mara moja kwa kushirikiana na Mshauri Elekezi wa Wizara, Dar Al-Handasah, ili kutekeleza majukumu yako ya kikimkataba. Kwa kumbukumbu nilizonazo, kazi hii kwa upande wa ujenzi katika saite, hususan umwagaji wa zege, ulianza kutekelezwa tarehe 25, mwezi wa 11, mwaka 2024. .Leo hii, tarehe 19, mwezi wa 7, mwaka 2025, ikiwa ni siku 236 baadaye, shughuli kubwa ya kumwaga zege takribani mita za ujazo elfu 50 inakamilika. Hii inadhihirisha umakini, weledi, na ustadi wa hali ya juu wa Mkandarasi."

Naibu Waziri aliendelea kusema kuwa kazi hiyo iliyotukuka ya mkandalasi inawapa tumaini kubwa Serikali na watekelezaji wa mradi huo, kuwa kazi itakamilika kwa wakati na kwa viwango tunavyotarajia. 

"Kwa kasi hii mliyoionyesha, Watanzania wanauhakika wa kuwa wenyeji wa mashindano ya AFCON mwaka 2027, nasi tunajivunia kusimama mbele yao tukiwadhihirishia, kwa vitendo, kuwa shauku yao itatimia. Mradi unatazamiwa kukamilika tarehe 24 mwezi wa 7 mwaka kesho, na tunaamini hilo linawezekana. Hii itatuwezesha kuutumia uwanja, kuujua na kujiandaa vizuri kabla ya mashindano ya AFCON."

Mwana Fa alieleza kuwa, mafanikio na kasi ya CRCEG mpaka kufikia hatua hii ni kutokana na ushirikiano ambao kwanza Serikali, kupitia Wizara yake ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, unauonyesha kwa kufanya malipo kwa wakati na kutoa ushirikiano katika vyombo vingine mbalimbali vya kiserikali vinavyosimamia shughuli hii pale unapohitajika. 

"Aidha, kwa kurahisisha shughuli za Mkandarasi za kitaalamu na usimamizi, natambua mchango mkubwa unaowekezwa katika utekelezaji wa mradi kupitia Mshauri Elekezi, Dar Al-Handasah, pamoja na Ofisi ya Msimamizi wa Wizara iliyopo hapa hapa site, yaani Clerk of Work. Vile vile tunatambua kuwa kuwepo kwa ofisi hizi katika mradi kunasaidia kuzitatua changamoto kwa wakati pindi zinapojitokeza, lakini pia kurahisisha utekelezaji na kusababisha Mkandarasi kujielekeza mojakwa moja katika utekelezaji wa mradi, " alisema Naibu Waziri na kusisitiza.

"Ushirikiano huu unazidi kujenga mahusiano yetu, kati ya mtu mmoja mmoja, makampuni ya kichina na ya wazawa kupitia mikataba midogo, wafanyabiashara na wataalamu wa ndanii inasaidia kuhamisha ujuzi na kubakiza ufanisi nchini, na pia inazidi kuimarisha mahusiano kati ya Serikali ya Tanzania na China.

Mwa Fa ambaye pia ni Mbunge wa Muheza alisema kuwa mradi huo ni mmoja wa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan. "Pongezi na asante nyingi zimfikie, anapoona juhudi hizi bila shaka zinamtia moyo na kuzidi kumuhakikishia kuwa thamani ya pesa na maono ya Serikali yake yana tija na kuwapa tumaini watanzania."

Alimalizia kwa kusema kuwa mradi huo ni wa kimkakati, unaodhamiria kuongeza chachu ya michezo nchini, ikiwa ni jitihada za makusudi kulea vipaji na kutengeneza jamii yenye nguvu na afya borakupitia michezo. 

"Niwatie moyo wakandarasi na wadau wote wanaohusika katika utekelezaji wa mradi huu; historia inajengwa, na tunayo kila sababu ya kujivunia kuwa miongoni mwa watekelezaji. Mradi huu ukaweke alama nyingine kubwa katika uhusiano kati ya Tanzania na China.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kenani Kihongosi amesema: "Nimekuwa nikiufuatilia kwa ukaribu sana mradi huu wa ujenzi wa uwanja mkubwa wa michezo jijini Arusha tangu ulipoanza kutekelezwa mwaka jana(2024). Sababu ya kuufuatilia mradi huu kwa ukaribu huo ni kutokana na kuwa miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa na Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 338 za Kitanzania zinawekezwa katika utekelezaji wa mradi huu."

RC aliongezea: "Lakini pia, mimi ni mdaumkubwa wa michezo, nikiamini kuwa michezo ni nguzo mojawapo ya kuimarisha afya na nguvu kwa vijana ambao ni taifa la kesho, na kwa Watanzania wote kwa ujumla."

Amesema kuwa anatambua kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 24 mwezi wa saba mwaka kesho. ", Mimi, kama ilivyokuwa kwa watangulizi wangu, nafurahishwa na juhudi zinazofanywa na mkandarasi katika utekelezaji wa mradi.

Kwa kasi ninayoiona, ni wazi kuwa mradi utakamilika ndani ya wakati, ili wakazi wa Arusha wawe wa kwanza kuutumia uwanja huu na kuonajuhudi inayofanywa na serikali yao,si kwa maneno tu bali kwa vitendo."

Aliongezea kuwa Arusha ni kitovu cha utalii, na uwanja huu ni kivutio kingine cha utalii wa michezo.

"Hivyo, naendelea kuwaasa wakandarasi na wadau wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa kujituma ili kukamilisha mradi kama inavyotarajiwa. Kiuchumi, natambua jinsi ambavyo shughuli za ujenzi wa uwanja huu umetengeneza ajira kwa vijana na wanawake wengi," alisema.

RC Kihongosi alisistiza; "Lakini pia, utakapokamilika, uwanja huu utazalisha ajira zaidi, kuibua biashara mpya zinazohusiana na michezo na burudani, kukuza sekta ya utalii, na kuchangia katika pato la taifakwa ujumla. Kwa hiyo, kwangu mradi huu ni wa muhimu sana, na nausubiria kwa hamu kubwa."

Aliwaeleza wakandarasi wanatekeleza mradi huo kuwa atendelea kuwapa ushirikiano katika masuala yote ya kiutawala, utaratibu, vigezo, na usimamizi unaotarajiwa kutolewa na ofisi yangu pamoja na taasisi zilizo chini yake ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa mafanikio na viwango.

"Aidha, nitoe rai kwa wadau wote wa utekelezaji wa mradi huu kusimamia kwa umakini, kwa uadilifu, na kwa uwajibikaji mkubwa fedha na muda wa utekelezaji, ili thamani ya fedha ionekane na maono ya Serikali yatimie. Mafanikio ya mradi huu yatakuwa sababu nyingine ya kuendeleza mahusiano kati ya Serikali ya Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China, " alisema.

Vilevile, amesema kuwa mradi huo umefungua fursa za kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo baina ya wataalamu na wakandarasi wa ndani, katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati kwa maslahi ya Taifala leo na la vizazi vijavyo.

Alimalizia kwa kusema: "Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha itaendelea kutoa ushirikiano wake kikamilifu ili kuhakikisha maandalizi ya mashindano ya AFCON yanafanyika kama yanavyotarajiwa, na kwa viwango vinavyokidhi matarajio ya nchi yetu.

Kwa dhati kabisa, nichukue fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais,Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa busara na wa kizalendo wa kuwekeza kwenye miundombinu ya michezo nchini,ikiwa ni sehemu ya kukuza vipaji, kuimarisha afya za Watanzania, na kulinda heshima ya nchi kimataifa."

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kampuni ya CRCEG Wang Yusheng amesema: "Kwa niaba ya CRCEG, napenda kutoa shukrani kubwa kwa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na serikali ya Tanzania kwa ukarimu, upendo, na msaada wao wakati wote tangu kuanza kwa mradi. Pia, nawashukuru vyema washauri elekezi, na timu zote zilizoshiriki katika ujenzi huu mpaka kufikia hapa. Zaidi ya hayo, ninawapongeza wafanyakazi wote waliojitoa usiku na mchana kwenye mradi huu mpaka kupelekea kazi hii kufikia hapa, tunawashukuru sana."

Yusheng aliongezea: " Tangu kuanza kwa ujenzi wa Uwanja huu wa Michezo mnamo tarehe 25 Julai 2024, chini ya uangalizi wa viongozi wetu na msaada wa wadau mbalimbali, tumeshinda changamoto nyingi. Kwa bidii ndani ya siku 360, tumefanikiwa kumaliza kazi ya zege kwa siku ishirini kabla, na haya ni mafanikio makubwa ya awali."

Amesema kuwa ujenzi wa uwanja huo ni mfano mzuri katika kuonyesha ushirikiano wa nchi ya China na Tanzania, na uthibitisho wa jitihada za CRCEG katika kuijenga "Mpango wa Mkanda Moja na Njia Moja”. Hii ni kuhakikisha uwanja unakamilika kwa ubora. Uwanja huu utakuwa jukwaa jipya la michezo wa mpira wa miguu, likisaidia Tanzania kukua kimichezo, kuboresha sura ya jiji, na kuvuta fursa za maendeleo. Pia kuleta mchango mpya kwenye uchumi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.

"Tunatambua kuwa hii ni hatua moja, lakini bado kuna hatua nyingine zaidi ili kukamilisha mradi huu. Hatua hii ya mwanzo ni mwendelezo wa jitihada mbalimbali ambazo tayari tumezianzisha. Huu ni ushaidi wa dhamira yetu ya kusonga mbele ili kufanikisha malengo ya mradi huu. Kwa dhima ya "Uhuru, Umoja na Kazi" ya Reli ya TAZARA, tutaendelea kufanya kazi kwa bidii, kupanua mipango, na kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati mnamo Julai 2026.

Mwisho, Nawatakia kila la kheri, katika majukumu yenu ya kujenga Taifa, na tunatarajia uwanja huu kukamilika ili utumike kama ilivyopangwa. Hii itachochea kuimarika kwa urafiki kati ya nchi ya China na Tanzania mara dufu. Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, Naibu waziri na wageni wote, nawatakia Afya njema na mafanikio makubwa.Asante.



Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...