Wana Ccm Kamnyonge,Nyamatare,Kwangwa Na Nyasho Wamuahidi Kumchagua Mathayo

GEORGE MARATO TV
0


Na Shomari Binda-Musoma 

WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Kata za Kamnyonge,Nyamatare,Kwangwa na Nyasho wamemuahidi kumchagua tena mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo uchaguzi ujao 2025.

Kauli hizo wamezitoa kwa nyakati tofauti leo juni 12,2025 wakati wa ziara ya mbunge huyo kwenye Kata hizo wakati akipita kuwashukuru kwa kumpa ushirikiano kwa miaka 5.

Licha ya kuahidi kumchagua wamemchangia fedha kwaajili ya kuchukua fomu kupitia chama hicho zitakazoanza kutolewa juni 28 mwaka huu.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kamnyonge Emanuel Bwimbo amemwambia mbunge huyo asiwe na shaka kwa kuwa yale aliyoyafanya wana kila sababu ya kumchagua.

Amesema wameridhika na utekelezaji wa ilani uliofanywa na mbunge huyo na hawana sababu ya kutokumchagua uchaguzi ujao.

Bwimbo amesema kwenye sekta ya elimu,afya,maji,miundombinu na masuala ya kijamii na Kata ya Kamnyonge wanakwenda kumchagua tena kuanzia ngazi ya chama hadi uchaguzi wa jumla.

" Mheshimiwa mbunge tukuahidi tuko pamoja na wewe na kwa nmna ulivyotekeleza ilani tutakwenda na wewe kwenye uchaguzi ujao.

" Na kwa kudhihilisha hilo tunakuchangia fedha ya kuchukua fomu na tutakuchagua tena muda ukifika usiwe na wasiwasi",amesema.

Kauli za kumuunga mkono mbunge huyo zimetolewa pia na wanachama wa Kata za Nyamatare,Kwangwa na Nyasho wakati alipofika kwenye Kata hizo.

Akizungumza kwenye Kata hizo mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amewashukuru wanachama hao kwa kuwa na imani naye na kumuahidi kumchagua tena muda utakapofika.

Amesema wamemuonyesha imani kubwa na kwa kuwa bado ana nguvu za kuwatumikia muda ukifika atachukua fomu kuwania tena nafasi hiyo.

Mbunge huyo amesema kabla ya kufanya ziara ya kushukuru alishasomaa utekeleza wa ilani na mengi yamefanywa kwenye sekta mbalimbali.

Ziara ya mbunge huyo itaendelea tena kesho kufika kuwashukuru wana CCM kwenye Kata ya Nyamatare,Makoko,Mukendo na Mwigobero.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top