Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb.) amempokea Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Museveni aliyewasili nchini Tanzania kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Februari 8, 2025.
Jumuiya zote mbili zinakutana kujadili kwa lengo la kupatia ufumbuzi hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.