Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania bara, Stephen Wassira amesema ili kutoingiza taifa kwenye migogoro kutokana na malalamiko ya wavuvi katika ziwa victoria upande wa wilaya ya Rorya mkoani Mara,ameshauri wavuvi kuvua kwa kuzingatia mipaka ya nchi na nchi.
Makamu mwenyekiti huyo wa CCM Tanzania bara, ametoa kauli hiyo februari 7,2025 wilayani Rorya, katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Mara baada ya kufanya ziara kama hiyo mkoa wa Geita na wilaya nyingine za mkoa wa Mara siku chache tu baada ya kushika wadhifa huo mkubwa katika hicho tawala.
Amewashauri wavuvi katika ziwa victoria wilayani humo na wilaya nyingingine kanda ya ziwa wanapofanya shughuli zao za uvuvi katika ziwa hilo, kuchukua tahadhari kwa kuacha kuingia kwenye mipaka ya nchi zingine ili kujiepusha na magogoro inaweza kuvuruga mahusiano na nchi jirani.
Wasira ametoa tahadhari hiyo baada ya kutolewa kwa taarifa matukio 12 ya wavuvi kuporwa na kunyang'anywa Mali zao ikisababisha na changamoto ya mipaka ya ziwa baina ya nchi na nchi.
"Hii changamoto ya uvamizi inatokana na kutokuwepo uaminifu baina ya wavuvi wenyewe wamekuwa wakigeukana wakati wa utekelezaji wa shughuli hii,ushauri wangu acheni kuingia kwenye maeneo ya nchi nyingine kwani mnaweza kuharibu mahusiano yetu"alisema Wassira
Kuhusu ujenzi wa barabara kuu katika wilaya hiyo,makamu huyo mwenyekiti amesema ataiomba serikali kuhakikisha inaharaikisha ujenzi wa barabara hiyo inayounganisha eneo la Mika- Kirongwe, Tarime-Serengeti pamoja na ya Musoma -Busekela kutoka na barabara hizo kuwa na umhimu mkubwa kwa uchumi wa Mkoa wa Mara.
Naye Mbunge jimbo la Rorya Jafari Chege alimuomba Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara Stephen Wasira kusukuma utekelezaji wa Mradi wa Maji wa miji 28 ili ukamilike ili usaidie wananchi kuondokana na changamoto ya ukosefu wa maji.
Pia amemuomba Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara Stephen Wasira kuangalia namna ya Tarura kuongezewa nguvu ya fedha ili kuwasaidia kutatua changamoto za Barabara kwenye maeneo hususani yanayoharibika.
Chege amempongeza Rais Samia kwa Miradi Mingi ambayo ameipeleka katika wilaya ya Rorya ikiwemo Vitui vya afya, Maji na ujenzi wa Barabara unaoendelea.
Amesema zipo Changamoto ambazo anatamani zikamilike ikiwemo mradi wa Maji katika kata za Kitembe na Roche wenye thamani ya zaidi ya Sh 400 milioni.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Ongujo Wakibara amesema chama cha Mapinduzi wilaya ya Rorya kinawapongeza wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kumchagua Wasira kwani ni kiongozi anayejua sasa za Tanzania.
Mwenyekiti huyo amemuahidi Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa kuwa katika uchaguzi Mkuu ujao hakuna kata itakayoenda upinzani ikiwa pamoja na kuhakikisha Mbunge wa Jimbo Hilo anashinda kwa kishindo