Mwandishi wetu ;Dodoma
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini Mwa Afrika ( MISA Tan) Bwana Edwin Soko Leo amemtembea Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Bwana Crispian Francis Chalamila na kufanya mazungimzo juu ya kufanya kazi Kwa pamoja likiwemo suala la kuendelea kuwashirikisha waandishi wa habari kwenye programu ya Marafiki wa TAKUKURU.
Hatua hii ni mwendelezo wa uongozi mpya wa bodi ya MISA Tanzania ya kuwatembelea wadau mbalimbali kwa lengo la kujitambulisha na kupanua uwigo wa kufanya kazi na wadau mbalimbali wakiwemo TAKUKURU
Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye ofisi za TAKUKURU Makao Makuu Dodoma