Anaandika Adrian Magoke Tizeba - Mwenyekiti Mstaafu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, 0754841003.
Wito kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu; Mchagueni Tundu Lissu Kukiongoza CHADEMA! Kwa nini?
1. Kwa sasa, CHADEMA ndiyo alama ya Upinzani katika Tanganyika na Taifa kwa ujumla.
2. Tanganyika na Watu wake, kwa sasa imekabwa kabali na Wezi na Wanyonyaji wa CCM ambao ni wabaya zaidi kuwahi kutokea, Hivyo inahitaji kukombolewa !
3. Kwa sasa 2025 na Kuliko wakati mwingine wowote, CHADEMA kinamhitaji Kiongozi madhubuti (yaani Mwanaume, Mtanganyika, Mzalendo wa kweli aliye tayari hata kufa kwa ajili ya nchi yake, mzoefu wa mapambano dhidi ya CCM, anayefahamika vilivyo nchini na Mwenye hofu ya Mungu) atakayeongoza vita ya CHADEMA ama Upinzani, Kuing'oa CCM Madarakani !
4. Kwa bahati mbaya sana, Mheshimiwa Freeman Mbowe sasa hivi, amepoteza sifa za Kuongoza Mapambano haya makali, mfano:
i. Ameishiwa pumzi na mbinu mpya hivyo lazima abadilishwe
ii. Anashukiwa kuwa ni dalali wa CCM na hivyo kuwa msaliti wa vita hii Takatifu
iii. Mbaya zaidi, anatumia rushwa kulazimisha kuendelea kuongoza vita hii, Jiulize sana, kwa nini afanye hivyo?!
5. Upande wa pili yupo Tundu Lissu:
Huyu ni damu changa na mpya kwenye nafasi hiyo ya kiongozi mkuu wa chama, Jasiri asiye na mfano, mkweli, mwelewa wa mambo mengi ya ulimwengu wa sasa, mwadilifu na mwenye sifa zingine zote zilizotajwa katika sababu ya 3 hapo juu.
Je, kama siye huyu Atakayeongoza vita hii, ni nani mwingine sasa?!
Au kama tulivyoambiwa, tumsubirishe Lissu hadi 2030?!
6. Wito wangu kwenu Wajumbe:
tazameni kwa mapana, pia tazameni mbali!kuleni hiyo rushwa ya Mbowe halafu mmuadhibu kwa kumpigia kura Lissu ili mjitofautishe na wajumbe wa CCM ambao kwa mtazamo wao finyu na mfupi, Wanakula rushwa na kupiga kura hukohuko!
Mkifanya hivyo, Mtakuwa mmechagua mabadiliko ya nchi yetu na mtabarikiwa sana maana Watanganyika na hata Wazanzibari wengi wanamtaka Tundu Antipas Lissu awe mwenyekiti wa CHADEMA leo, leo, leo
Mkumbuke, mkichagua kwa usahihi, majina yenu yataandikwa ukurasa wa Kwanza wa Historia ya Ukombozi wa nchi yetu,
Ahsanteni sana leo nikomee hapo, nitaandika tena baada ya uchaguzi !