Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali Kuchukua hatua kali kwa Watu Wanaohujumu Miundombinu ya Umeme


📌Dkt. Biteko azindua mradi wa usafirishaji umeme (kV 400) Chalinze - Dodoma  na upanuzi wa vituo vya umeme Chalinze na Zuzu

📌Kuwezesha umeme kutoka JNHPP kufika Kanda mbalimbali za Tanzania, Migodi ,Viwanda, Kusini na Mashariki mwa Afrika

📌Asema Tanzania inaongoza Afrika kwa Usambazaji wa umeme kwa wananchi

📌Apaza sauti kwa wahujumu wa miundiombinu ya umeme; ataka hatua kali zichukuliwe


Leo Tanzania imeandika historia nyingine katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya umeme baada ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Doto Biteko kuzindua utekelezaji wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma  na upanuzi  wa vituo vya kupoza umeme vya  kilovoti 400 Chalinze-Pwani na Zuzu-Dodoma.

Mradi huo wa umeme uliozinduliwa utawezesha umeme wote unaozalishwa katika mradi wa kuzalisha umeme wa JNHPP kufika katika maeneo yote ya mikoa iliyopo Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kati, Kanda ya Magharibi, Migodi, Viwanda na kuimarisha biashara ya umeme Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Dkt. Biteko amesema kutekelezwa kwa mradi huo  kunatokana na Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali pamoja na miongozo yake ya namna bora ya kutekeleza miradi ili kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa uhakika kwa lengo la kukidhi mahitaji ambayo yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku kutokana na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Amesema kuwa kutokana na jitihada hizo zinazofanywa na Rais Samia katika kuendeleza miradi ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme imepelekea Tanzania kuwa kinara barani Afrika katika usambazaji wa umeme kwa wananchi na hii ni kutokana na takwimu zilizotolewa na Benki ya Dunia.

Ameeleza  kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea na jitihada za kuimarisha upatikanaji wa nishati ya umeme nchini ambazo zimewezesha kuongeza uwezo wa mitambo ya kufua umeme iliyopo nchini hadi kufikia Megawati 3,169.26 ambapo mahitaji ya juu ya umeme nchini kwa sasa yamefikia Megawati 1,888.72 ambapo mahitaji hayo hayajawahi kufikiwa kutoka nchi ipate Uhuru na hii ikimaanisha kuwa uchumi unazidi kukua kutokana na kuongezeka kwa shughuli za maedeleo. 

“Kuimarika kwa uzalishaji wa umeme nchini kumechangiwa na  kuanza uzalishaji katika Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 ambao hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 99.6 na jumla ya Megawati 1,175 za umeme zinazalishwa na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa. “Amesema Dkt.Biteko.

Katika Hafla hiyo, Dkt.Biteko amekemea vikali wahujumu wa miundombinu ya umeme ambao amesema kuwa wanarudisha nyuma uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika kuwafikishia wananchi nishati ya uhakika na kuagiza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua kali kwa wahujumu hao ambao oia wamekuwa wakikosesha wananchi umeme pale miundombinu inapoharibiwa.

Kuhusu Wakandarasi wa mradi huo, Kampuni ya TBEA kutoka China, amewataka wahakikishe mradi  unakamilika kwa wakati ili wananchi wapate manufaa yaliyokusudiwa ikiwa pia ni maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dkt.Biteko ametumia hafla hiyo kuwakumbusha viongozi na wananchi kuhusu jitihada za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kutimiza lengo la Serikali la asilimia 80 ya Watanzania  kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Katika muendelezo wa jitihada hizo, amesema Serikali imetoa ruzuku kwa mitungi ya gesi zaidi ya 400,000 itakayouzwa kwa nusu gharama ya bei ya soko ambapo mitungi hiyo inasambazwa katika Mikoa yote Tanzania Bara.

Ametoa wito kwa Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia kwa kutumia majiko ya gesi na teknolojia mbalimbali kulingana na mazingira ikiwemo nishati ya umeme kwani nishati hizi ni miongoni mwa nishati safi, salama na ya gharama nafuu ikilinganishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Vilevile ametoa wito kwa wadau mbalimbali na wafanyabiashara nchini kuhakikisha majiko yanayotumia nishati fanisi ya umeme yanapatikana kwa wingi na kwa bei nafuu ili wananchi wengi katika maeneo mbalimbali wakiwemo wa vijijini waweze kutumia umeme kwa ajili ya kupikia.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Innocent Bashungwa ameipongeza Wizara ya Nishati na TANESCO kwa uzinduzi wa mradi huo  wa usafirishaji umeme na upanuzi wa vituo vya kupoza umeme vya  Zuzu Dodoma na Chalinze na kueleza kuwa utekelezaji wa mradi huo unaakisi dhamira ya Rais Dkt. Samia ya kutaka watanzania wapate nishati ya uhakika.

Bashungwa amesema kuwa Serikali inatoa fedha nyingi ili kutekeleza  miundombinu ya umeme hivyo Wizara yake itahakikisha miundombinu hiyo inalindwa kwa wivu mkubwa na kuwashughulikia wahalifu wa moundombinu hiyo,


Kwa uoande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amempongeza Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanyika katika Sekta ya Nishati na pia amempongeza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt.Doto Biteko kwa kusimamia Sekta kwa weledi, ufanisi, uzalendo na uchapakazi wa hali ya juu.


Amesema mradi uliozinduliwa leo ni muhimu kwani Tanzania inategemewa kuimarisha hali ya umeme kwa nchi za Mashariki mwa Afrika kupitia miradi ya uzalishaji na usafirishaji umeme ambayo inaendelea kufanyika.


Amesema moja ya masuala yaliyokuwa yakitiliwa mkazo katika  Mkutano uliohusu biashara ya kuuziana umeme na kununua umeme kwa nchi Wanchama Mashariki mwa Afrika (EAPP) ni uunganishaji umeme kati ya Tanzania na Kenya  ambapo leo  laini hiyo ya umeme ya kV 400 imewashwa na pongezi zimetolewa kwa Rais Samia na Dkt.Biteko kwa kutekeleza mradi huo.


Kwa upande wake, Katibu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema sasa nchi inazalisha zaidi ya megawati 3000 za umeme na hii inaifanya Tanzania kuwa nchi inayozalisha umeme mwingi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki na hivyo kutoa fursa kwa Tanzania kufanya biashara ya umeme na nchi nyingine za Afrika iikwemo Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya.

Amesema mradi huu utaenda katika kanda mbalimbali ikiwemo mikoa ya Kaskazini na kuingia hadi nchini Kenya.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga alisema mradi wa kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma umegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni  ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme katika msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma yenye urefu wa kilomita 345 na upanuzi wa vituo vya kupokea na kupoza Umeme vya Chalinze (400/220/132kV) mkoani Pwani na Zuzu (400/220/33kV) Mkoani Dodoma.

Alisema  malengo ya mradi huo ni kuwezesha usafirishaji wa umeme wote (2,115MW) utakaozalishwa katika Bwawa la JNHPP na kuufikisha kwenye maeneo yote ya mahitaji ya umeme, hatua itakayosaidia kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme kwenye Gridi ya Taifa na kuongeza uwezo wa kusafirisha umeme kwenda mikoa yenye viwanda na migodi ya uchimbaji madini ya Kaskazini Magharibi, Kaskazini Mashariki, Kanda ya Kati na Kusini mwa Tanzania.

Alieleza kuwa, lengo lingine la mradi ni kuwezesha zoezi la uunganishaji umeme kwa pamoja katika mifumo ya Mashariki mwa Afrika (Eastern Africa Power Pool - EAPP) na Kusini mwa Afrika (Southern Africa Power Pool - SAPP) na hivyo kuwezesha kufanyika kwa biashara ya nishati ya umeme kikanda (Regional Power Trading).

Aliongeza kuwa, Mradi husika unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 kwa jumla ya gharama ya Shilingi 513 Bilioni ambapo Mkandarasi  Kampuni ya TBEA kutoka China  ameshalipwa malipo ya awali ya kiasi cha Shilingi bilioni 107.93 ambayo ni asilimia 20 ya gharama za mradi.

Alieleza kuwa katika mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme, kazi mbalimbali zimeanza na mradi utakamilika mwaka 2026 mwezi Septemba huku mradi wa upanuzi wa vituo vya kupoza umeme kazi pia zinaendelea na mradi utakamilika Septemba 2026.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amesema mradi huo ni uthibitisho wa kazi kubwa na nzuri za Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwamba umeme huo utafaidisja Tanzania na nchi nyingine za Afrika na ni sehemu pia ya uhamasishaji wa nishati safi ya kupikia kwani wananchi watatumia umeme huo kupikia.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amesema wananchi mkoani Morogoro wanatambua  kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia katika kuendeleza miradi ya umeme ikiwemo kukamilisha miradi ya miaka mingi ukiwemo wa kuunganisha umeme kati ya Tanzania na Kenya.

Mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo katika hafla hiyo, Wendy Hughes ambaye ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia  Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kujikita katika kuiimarisha gridi ya taifa ya umeme ambayo ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii pamoja na kutoa uhakika wa usalama wa nishati.

Amesema kuwapo kwa mifumo imara ya usafirishaji umeme itafanya wananchi kufikishiwa umeme wa uhakika katika maeneo mbalimbali ya nchi na pia   ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa kufikisha umeme kwa watu milioni 300 barani Afrika ifikapo 2030.

Ameahidi kuwa Wadau wa Maendeleo wataendelea kutoa  ushirikiano kwa Tanzania ili kukamilisha mipango mbalimbali ya maendeleo ambayo nchi imejiwekea.






Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...