Kufeli Kwa Breki Chanzo cha ajali iliyosababisha vifo vya watu 11 Kagera

GEORGE MARATO TV
0



Na Angela Sebastian; Bukoba 

Watu 11 wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya basi ya kampuni ya Copco one yenye namba za usajili T857DHW aina ya Scania linalofanya safari zake kutoka Kigoma kwenda mjini Bukoba kufeli breki wakati limesimama kumshusha abiria na kuanza  kurudi kinyumeyume na kuacha njia kisha kupinduka.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa alieleza hayo (leo) jana wakati akiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ofisini kwakwe mjini Bukoba ambapo alisema ajali hiyo imetokea jana jumamosi Desemba 21,2024 majira ya saa nane mchana katika kijiji cha Kabukome kata Nyarubungo eneo la mlima wa pori la Kasindaga wilaya ya Biharamulo.

Hajat Mwassa alisema gari lenye namba za usajili T857 DHW Scania basi mali ya Roja line travel company Ltd likiendesha na Saidi Mkenda (41) likitokea mkoani Kigoma kwenda Bukoba ambapo, dreva huyo alisimama kushusha abiria ambae alikuwa mtoto aliyepitilizwa kwenye kituo, ndipo gari lilisima ila liliashindwa kupanda mlima na kurudi nyuma kisha kuingia mtaloni na kupinduka na kusababisha vifo 11.

"Katika vifo hivyo wanawake sita,wanaume wanne na watoto wawili tumepokea kwa masikitiko makubwa sana ukizingatia ndani ya kipindi kifupi tumepata ajali mbili zilizochukua maisha ya watu wengi siku chache zilizopita iliyokea ajali mbaya Wilayani Karagwe na hii ya jana hivi natumia fursa hii kutoa pole kwa wananchi wa mkoa wa Kagera na ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao"alieleza kwa masikitiko RC

Alitoa ombi kwa wananchi wa mkoa huo hasa madreva kuwa waangalifu wanapoendesha magari ya abiria na binafsi hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambapo kunakuwa na ajali nyingi hivyo aliagiza polisi kitengo cha Usalama barabarani kufanya ukaguzi wa magari kabla ya kuanza safari kuhakikisha usalama na uzima wake na spidi zinazoendeshwa ziwe zinazoruhusiwa.

Alisema pia majeruhi 16 walilazwa katika hispitali teule ya Biharamulo ambapo 12 mchana huu wameruhisiwa na wanne akiwemo dreva wakiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Kamanda wa polisi mkoani kagera Blasius Chatanda alisema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali hiyo ni  ubovu wa gari hpilo na uchuguzi zaidi unaendelea.

Aidha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa alifika eneo ilipotokea ajali  na kuwajulia hari majeruhi waliolazwa katik hospitali y Biharamulo.

Akizungumza baada ya kutembelea majeruhi, Waziri Bashungwa hapo jana alitoa  pole kwa  familia, ndugu na jamaa wote walioguswa na ajali hiyo na kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwaombea majeruhi wapone haraka.

Kwa Upande wake, Mganga mkuu wa Hospitali teule ya Biharamulo, Gresmus Sebuyoya alieleza kwa majeruhi 26 waliruhisiwa jana na wengine 16 wanaendelea na matibabu na ungalizi wa karibu. 










Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top