Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wasifu wa Jenerali mstaafu David Musuguri

 

Jenerali mstaafu David Bugozi Waryoba Musuguri alizaliwa Januari 4, ‌1920 katika Kijiji cha Kumuruti,Masabha.Sasa sehemu hiyo inajulikana kama Nyasirori, akiwa mtoto wa tatu katika familia ya mzee Musuguri wa Nzangho.

Alipozaliwa aliitwa jina la Waryoba,ikiwa ni ishara kwamba alizaliwa asubuhi wakati jua linachomoza. Baba yake mkubwa, Mgendi wa Nzangho alimwita jina la Bugingo.

Akiwa na umri wa miaka mitano, mzee Musuguri Nzangho alihamia Kijiji cha Butiama‌, ‌wakati huo paliitwa ‌Mu-kyaro.

Jenerali mstaafu David Bugozi Waryoba Musuguri alikuwa mtoto wa tatu kuzaliwa katika tumbo la mama yake, Wakuru wa Kibumbiko.Bibi mzaa mama yake pia alikuwa anaitwa Wakuru wa Kigeso. Jina la Wakuru ni jina kubwa sana katika ukoo huu wa Jenerali Musuguri.

Mzee Musuguri wa Nzangho alioa wanawake ‌sita. Alikuwa mfugaji wa ng’ombe na mbuzi na alikuwa stadi kulinda mifugo yake, kwani yeye na wachungaji wenziwe waliwahi kwenda kuwinda simba na waliua simba 18‌.

Enzi hizo wanyamapori walikuwa wapo mapori ya karibu maeneo ya ‌Bisarye, Ikizu na Buhemba.

Akiwa kijana mdogo, hakubahatika kwenda shule. Muda mwingi alichunga ng’ombe na mbuzi wa baba yake, kwa kuwa alikuwa mtoto wa kiume pekee hapo kwao, wengine walikuwa wasichana.

Jina la Bugozi Jenerali Musuguri kwa maisha yake ya kazi amejulikana pia kwa jina la Bugozi. Jina hili alijiita mwenyewe kutokana na uwezo wake wa kupigana mieleka, inayojulikana kwa Kizanaki kama, ‘erigori.’ Wakati huo ‘erigori‌’ lilifanyika eneo ambalo lilipata umaarufu kwa kuitwa jina lake hilo.

Kuingia Jeshi la Mkoloni – King’s African Rifles (KAR) Jenerali Mstaafu Musuguri aliingia jeshini ‌katika mazingira tata. Mwenyewe anasimulia kwamba kati ya mwaka 1942 au 19‌43, katika sehemu ya kilima cha Mutuzu‌, ‌Butiama kuna mama aliuawa kutokana na sababu za kishirikina. Polisi walifika ‌hapo kijijini na kuwakamata vijana ili wasaidie kubeba mwili wa marehemu ‌kuupeleka Musoma kwa ajili ya uchunguzi.

Wakati wakisubiri kwenda Musoma‌, ‌waliwekwa rumande kwenye boma la Chifu Edward Wanzagi Nyerere. Lakini usiku kabla ya safari hiyo‌, ‌kijana Waryoba Musuguri akiwa na umri wa miaka 22, na vijana wengine walitoroka na kwenda Musoma‌. Huko akajiandikisha kujiunga katika Jeshi la KAR.

Alipotoroka aliambatana na wenzake – ‌Mugendi Nyamatwema na Mkono wa Nzenzere. Wakatembea mpaka Musoma kujiunga jeshini.

Wakati huo Chifu Edward Wanzagi Nyerere alikuwa ametawazwa mwaka 1942 baada ya baba yake, Chifu Nyerere Burito, kufariki dunia.

Baadaye alijiunga na vijana wenziwe Mwanza, wengine wakajiunga Morogoro, mpaka walipo‌fika ‘depo’ ya mafunzo Dar es Salaam.

Akiwa jeshini ndiko alikopata elimu ya kusoma na kuandika, na akaweza kujiendeleza hata kufanya kozi ‌mbalimbali za kijeshi katika nchi za Canada na China.

Akiwa KAR alipigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia ambayo ilimwezesha kupigana katika uwanja wa vita katika nchi nyingi, zikiwamo India, Burma, Ushelisheli, Canada, mpaka Japan ambako alijeruhiwa kwa risasi kwenye paja. Alivuja damu na kupoteza ‌fahamu‌. Alibebwa na askari mwingine Mtanzania aliyeitwa Marega – huyu anatoka Ngoreme. Kwa kitendo hicho cha kumwokoa, aliendelea ‌kuwa rafiki yake wa karibu hadi alipofariki dunia.

Akiwa KAR‌, miongoni mwa wanafunzi wake ni aliyekuja kuwa kiongozi wa Uganda, ‌Idd Amin Dada, aliyejiunga na jeshi la KAR, Kahawa Barracks mjini Nairobi.

Jenerali ‌Musuguri pia alipigana vita ya MAUMAU nchini Kenya baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia akiwa jeshi la KAR.

Mwaka 1957 aliongoza kikosi cha wanajeshi wa KAR kutoka Afrika Mashariki kwenda London, Uingereza kwenye gwaride la Malkia wa Uingereza. Alipeleka ‌historia ya KAR katika Afrika Mashariki, na yeye ndiye aliyemkabidhi historia hiyo Malkia Elizabeth II Juni 11, 1957 katika Kasiri la Mfalme la Buckingham wakati huo akiwa na cheo cha Warrant Officer Platoon Commander (W.O.P.C). Alikuwa Mwafrika wa kwanza kuonana na kupeana mkono na Malkia Elizabeth II wa Uingereza.Uhuru

Baada ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 1961, aliendelea kuwapo jeshini. Baada ya Uhuru KAR ilibadilishwa jina na kuitwa Tanganyika Rifles.

Baada ya maasi ya mwaka 1964, Jeshi la Tanzania liliundwa upya likawa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ‌) ‌au Tanzania People’s Defence Forces (TPDF)‌, ‌likiwa na viongozi Watanzania wazalendo. Alikwenda kwenye vita ya Kagera ya kumtimua nduli Idd Amin ‌kati ya mwaka 1978 hadi 1979, ambako alitambulika kwa kuongoza vita kishupavu na akaitwa ‘‌Jenerali Mutukula, ‌Kamanda mwenye Uso wa Chuma’.


Jenerali mstaafu ‌Musuguri alipitia vyeo vyote vya kijeshi kuanzia ‘Private’ mpaka ‘‌Full General’ akiwa Mtanzania wa kwanza kupata cheo hicho cha ‘‌Full General’.

Aliendelea kufanya kazi ya jeshi kwa weledi na ujasiri hadi alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ‌(CDF). Kwa mtiririko wa ma-‌CDF wa JWTZ, Jenerali Musuguri alikuwa ‌wa tatu.

Alistaafu kazi ya jeshi mwaka 1988 na tangu hapo amekuwa akiishi nyumbani kwake Butiama akijishughulisha na kilimo na ufugaji.


                        

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...