Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mtambi awataka Wananchi mkoa wa mara kuchangamkia fursa chuo cha Mjnuat


 Shomari    Binda-Butiama    

MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi  amewataka wananchi wa mkoa huo  kuchangamkia fursa za uwekezaji chuo kikuu  cha kilimo cha  Mwalimu Nyerere  ( MJNUAT)     

Fursa zilizotajwa ni  pamoja na ujenzi wa  miundombinu  dmbalimbali ikiwemo ya   huduma kwenye  mazingira ya chuo. 

 Hayo ameyasema   katika Wilaya ya Butiama     baada ya serikalik uwekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu cha Mwalimu  Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT ).   

Akizungumza baada  kushuhudia utiaji saini   wa mkataba wa ujenzi  wa miundombinu d mtambuka wenye   thamani ya shilingi bilioni 9 katika  chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) na mkandarasi Shandong Hi-Speed Dejian Group Co. Ltd na Mshauri  mwelekezi Epitome  Architects Limited.

 Mtambi amesema fursa zinazotokana na uwepo na Chuo hicho kwa Mkoa wa Mara ni nyingi zinazo dhitaji uwekezaji.

“Niwaombe wananchi wa mkoa wa  Mara na atanzania wote kwa ujumla kuchangamkia fursa uwepo wa Chao hiki kuwekeza katika biashara mbalimbali  kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi na watumishi wanaotegemewa kuwepo katika Chuo hiki”,amesema.

Amesema kutokana maamuzi ya serikali kukifanya Chuo hicho kibebe sehemu ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa Chuo hicho na ambacho amesema kitakapokamilika kitaleta mapinduzi makubwa ya kijamii na kiuchumi katika Mkoa wa Mara. 

“Chuo hiki kinasadifu shabaha halisi ya kumuenzi Baba wa Taifa na kama Mkoa tunaishukuru Serikali kwa maamuzi yake ya kujenga Chuo hiki  Mkoa wa Mara, huu ni mmoja kati ya miradi mikubwa ya kimkakati hapa nchini” ameongeza.

Mtambi amekipongeza Chuo kwa kujenga majengo na miundombinu mtambuka ambayo it's borders  zaidi eneo hilo na kuifanya miundombinu iliyokuwepo na inayoendelea kujengwa katika eneo hilo itumike kiurahisi zaidi na ujenzi utakapokamilika iweze kutoa huduma stahiki. 

Amewataka wakandarasi walioshinda zabuni mbalimbali za ujenzi wa   miundombinu ya  Chuo hicho kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakamilika kwa wakati ili miundombinu inayojengwa iweze kutumika na kuwahakikishia kuwa Mkoa utatoa ushirikiano unaohitajika katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo.   

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la MJNUAT Ndugu Philemon Luhanjo amesema Chuo hicho kitakapokamilika na kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi wengi na hivyo kuleta matokeo  chanya katika Mkoa wa Mara na kuwaomba wananchi kutumia fursa hiyo kuwekeza.  

“Ninashukuru sana kwa ushirikiano ambao Chuo hiki unaupata kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama na viongozi wengine katika Mkoa wa Mara” amesema Ndugu Luhanjo na kuongeza kuwa ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho inategemewa kukamilika mapema mwakani kama mikataba ya ujenzi inavyoonyesha. 

Luhanjo ameipongeza Menejimenti ya Chuo kwa usimamizi mzuri wa mikataba ya ujenzi na kuwezesha kufikia wastani wa asilimia 43 ya ujenzi wa majengo 15 ambayo ni sehemu ya miundombinu ya Chuo hicho katika Kampasi Kuu. 

Ndugu Luhanjo ametumia nafasi hiyo kuwataka watumishi na viongozi wote wa Chuo hicho kutimiza wajibu wao kikamilifu kwani wamepata bahati ya kuwa katika waanzilishi wa Chuo hicho ili waweze kuandaa mazingira mazuri kwa watu wengi zaidi kujiunga na chuo hicho.  

Ndugu Luhanjo amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa Chuo hicho kitafuatilia na kuhakikisha ujenzi wa miundombinu hiyo yote unafanyika kwa mujibu wa mkataba na makubaliano yaliyofikiwa.  

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lesakit Mellau ameeleza kuwa mradi wa miundombinu mtambuka ni sehemu ya mradi mkubwa wa shilingi bilioni 102.5 za mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ambapo katika ujenzi wa majengo ya mradi huu umeanza na unaendelea vizuri. 

“Katika mradi huo uliofadhiliwa na Benki ya Dunia, MJNUAT kimepata fedha ambazo ni sawa na asilimia 10 za fedha zote zilizotolewa kwa taasisi nyingine 22 za Elimu ya Juu hapa  nchini, hili ni jambo la kujivunia sana” amesema Prof. Mellau. 

Prof. Mellau ameeleza kuwa ujenzi wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia kwa sasa unaendelea vizuri na umefikia wastani wa asilimia 43 na Chuo kinategemea ujenzi wa miundombinu mtambuka pia utatekelezwa kwa muda uliopangwa na kukamilika ndani ya muda uliowekwa katika mkataba wake.   

Prof. Mellau amesema ujenzi utakapokamilika Chuo hicho kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi hadi 4,500 kwa Kampasi Kuu, wanafunzi 600 katika Kampasi ya Oswald Mwang’ombe na wanafunzi 1,500 kwa Kampasi ya Tabora na kinatarajiwa kuwa na wastani wa watumishi 700.  R

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi huo kutoka MJNUAT Mkadiriaji Majenzi (QS) Osward Bujiku ameeleza kuwa mradi huo ambao ni sehemu ya mradi mkubwa unafadhiliwa na Benki ya Dunia na unategemewa kutekelezwa kwa muda wa miezi kumi na utagharimu shilingi 9,093,848,880.98. 

QS Bujiku ameeleza kuwa mradi wa miundombinu mtambuka utahusisha ujenzi wa mfumo wa maji na ufungaji wa mfumo wa maji taka, ujenzi wa miundombinu ya michezo, ufungaji wa mifumo ya umeme, ujenzi wa barabara za ndani na ujenzi wa miundombinu katika shamba la mfano la Chuo hicho.  

Bwana Bujiku ameeleza kuwa miundombinu mingine itakayojengwa katika mradi huo ni lango kuu la kuingilia Kampasi Kuu ya Chuo hicho, ujenzi wa kichomea taka kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Chuo hicho ujenzi wa kingo za kulinda maeneo ya mabonde yoliyomo katika eneo hilo.  

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Ludovick Kaegele, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Butiama, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Agness Mwakaje, Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Mipango na Utawala Dkt. Abubakari Said Mgelwa, Menejimenti na watumishi wa Chuo hicho.



Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...