Serikali kujenga vituo vya zana za kilimo nchi nzima

GEORGE MARATO TV
0


Serikali imetangaza kujenga vituo vya zana za kilimo nchi nzima pamoja na kuanza kugawa ruzuku ya mbegu za mahindi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati wa ziara yake katika kituo cha ununuzi wa mahindi Madaba ambapo ameahidi kula sahani moja na walanguzi wanaowanyonya wakulima nchini. 

Amesema kuwa Serikali inatambua adha wanayokutana nayo wakulima kutokana na uhaba wa Zana za kilimo pamoja na maumivu yatokanayo na kukodi Trekta, pawatila pamoja ulanguzi katika mbegu na mbolea.

“Rais Samia Suluhu Hassan kwa nia ya dhati kabisa ameamua na kutenga fedha za kujenga zaidi ya vituo 45 vya zana za kilimo nchi nzima ili kutatua changamoto zinazowakabili wakulima,”amesema.

Vituo hivyo vitakuwa na zana za kilimo kama matrekta na zana zake zikiwemo plau, haro, planters, boom sprayers na tela za kusafirishia mizigo pamoja na Combine Harvester

Waziri Bashe ameitaja mikoa itakayonufaika na awamu ya kwanza ya ujenzi huo kuwa ni Mwanza,Simiyu,Geita,ShinyangKigoma,Mara,Tabora,Singida,Katavi,Shinyanga,Mbeya, Njombe, Ruvuma, Tanga, Dodoma.

“Tumetambua kuwa wakulima wanakodishiwa zana hizo kutoka sh. 60,000 hadi 120,000 hii si sawa na  kuumiza wakulima na hawawezi kuona tija katika kilimo,hivyo Serikali imeamua italeta zana hizo ikiwemo matrekta na wakulima watakodi kwa bei elekezi ya sh 35,000 hadi 40,000 haitazidi hapo,”amesema.

Aidha Mwakani Serikali itasambaza mashine za kusafishia mahindi, mtama na mazao mengine lengo ni kuona bidhaa hizo zinakidhi viwango vya soko la kimafaifa na itatenga fedha ya kununua Mazao yasiyo na ubora kwa ajili ya chakula cha mifugo ili kuwapunguzia hasara wakulima. 

Pia waziri Bashe ametangaza vita na wafanyabiashara wanaowanyonya wakulima hususani wanaonunua mazao kwa bei ya chini na wanaouza pembejeo za kilimo kwa bei ya ulanguzi.

“Wapo wafanyabishara wanaokula jasho la wakulima bila uoga,bei elekezi ya mahindi ni sh 700 kg lakini wao wananunua kwa sh 300, mpunga kg 1 ni sh 900 kg 100 sh 81,000 wao wananunua kg 1 kwa sh 600,hii haikubaliki"alisema Waziri Bashe na Kuongeza kuwa

“Sina tatizo na wafanyabishara lakini sitavumilia unyonyaji uliopitiliza tutajenga maghala kila sehemu hawataki kununua naiagiza Mamlaka ya Hifadhi ya Chakula (NFRA), kuhakikisha inanunua mazao hayo nchi nzima mpaka kabla ga msimo wa kilimo kuisha"

Naye Mbunge wa Madaba Dkt. Joseph Mhagama akizungumza kwa niaba ya wananchi, ameishukuru serikali kwa hatua zinazoendelea ikiwepo ujenzi wa ghala kubwa katika kata ya Madaba na ujenzi wa vituo 9 vya zana za kilimo mkoni humo.

“ Sisi Madaba tumejiandaa kupokea neema hiyo na tumetenga zaidi ya hekari 25,000 za ardhi kupisha eneo la zana za kilimo na mashamba ya mbegu,”amesema









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top