Mradi wa Ujenzi wa Tawi Jipya la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Katika Wilaya ya Bukoba Wafikia Asilimia Kumi

GEORGE MARATO TV
0


Na Angela Sebastian-Bukoba

UJENZI wa tawi  jipya la Chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia mradi wa elimu ya juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaoendelea mkoani Kagera umefikia asilimia 10 tangu uanze mwezi Julai mwaka huu.

Mradi huo unajengwa katika kata ya Karabagaine Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ambapo, mradi utawezesha huduma ya elimu ya juu kuwafikia watu wengi katika maeneo ambayo ni nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari katika eneo unapojengwa mradi huo Naibu Mratibu wa mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk.Liberato Haule amesema walikabidhi mradi kwa mkandarasi mwezi Mei na ujenzi ulianza rasmi mwezi Julai mwaka huu ambao unajumuisha madarasa,kambi za mihadhara,ofisi za walimu na mabweni kwa ajili ya wanafunzi.

"Kwanini tumeamua kuanzisha miradi hii ya ujenzi huu ni kuhakikisha tunasogeza zaidi huduma ya chuo kikuu cha Dar es Salaam kwenye maeneo ambayo ni nje ya Dar es Salaam na ambapo hatujawahi kufika hivyo, tunajenga matawi mawili ambayo moja ni hapa Kagera itakayoangazia shughuli za biashara na nyingine mkoani Lindi ambayo itashughulika na masuala ya kilimo"amesema Haule 


Hule amesema chuo hicho kinachojengwa Kagera ni kwa ajili ya shule ya kufundisha masuala ya biashara ambapo ni sambamba na miradi mingine miwili inayojengwa Lindi na Zanziba ambayo kwa pamoja ikikamilka itasaidia ongezeko la madarasa na kubeba idadi kubwa ya wanafunzi.

Amesema kwa sasa chuo kimepiga hatua katika mageuzi ya mitaala pamoja na mbinu za kujifunzia baada ya kufanya ufuatiliaji wa wahitimu wao kwa kutumia kamati za tasnia pamoja na kupokea maoni, kwenye vituo vikuu vya kimataifa huko nje pamoja na wadau ambao ndio waajiri ndipo wakafikia uamizi wa kuboresha mitaala iliyopo na kuunda mitaala mingine mipya ipatayo 18.

Aidha dk. Haule alieleza kuwa wameunda mifumo ya kidigitali ambayo itawasaidia kila mtu  kupata nafasi ya kusoma katika mazingira aliyopo bila kumlazimisha mwanafunzi kuhudhuriwa eneo la chuo pia itawajenga vyema wanapomaliza masomo yao waweze  kuendana na ushindani wa soko la ajira.

Dk.Paulo Ndumbaro mtaala wa miundombinu hasa majengo kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam alisema mradi huo unatarajiwa kujengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 13.1 na kukamilika mwezi  Novemba 2025 kwahiyo akawshauri wananchi wajiandae kutumia fursa hiyo ikianza.

Naye Mkandarasi mshauri mhandisi Leonard Mwamboka amesema kwasasa wapo katika hatua ya ujenzi wa msingi ambapo wamefikia asilimia kumi ya ujenzi hivyo,wanajitahidi kuhakikisha mkandarasi anatekeleza mradi kulingana na matakwa ya mkataba,ubora na kukamilisha kwa wakati.

Afisa mipango miji na vijiji Halmashauri ya Bukoba Bluno Barongo amesema eneo linalotarajiwa kujengwa chuo hicho lilitolewa na vijiji viwili vya Kangabusharo na Itahwa  hekari 315 ambapo tiyali limepimwa na na kupewa hati miliki na kamishna wa ardhi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top