Mradi wa kimkakati wa ujenzi wa soko kuu la Mwanza wafikia asilimia 96

GEORGE MARATO TV
0


Ujenzi wa soko kuu la mwanza unaotekelezwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi billioni 23 umefikia asilimia 96

Waziri wa fedha Dkt.Mwigulu Nchemba amekagua maendeleo ya ujenzi wa soko hilo la kimkakati na kueleza kuridhishwa kiwango cha ubora wa kazi. 

Dkt.Nchemba amesema kuwa soko hilo ambalo ujenzi wake utakamilika hivi karibuni utaboresha mazingira ya biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi. 

Aidha amemtaka mkandarasi kampuni ya Mohamed builders kukamilisha ujenzi wa soko hili kwa wakati ili wananchi wa mwanza waweze kunufaika kiuchumi na uwepo wake.

"Hatua ya ujenzi iliyofikiwa na soko hilo ni kielelezo cha uthubutu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii,Niwaombe watanzania wenzangu tuendelee kumuunga mkono kwa kumchagua kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ili aendeleze Jitihada za kuleta maendeleo"alisema waziri Mwigulu

Kaimu mkurugenzi wa Jiji la mwanza Erick Mvati akitoa taarifa kuhusu mradi wa ujenzi wa soko kuu la Mwanza amesema mradi huo unalenga kuboresha miundombinu ya masoko pamoja na kuongeza mapato ya jiji.

Mvati amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutawezesha wa fan ya biashara elfu moja na Mia nne kufanya biashara zao katika mazingira rafiki ikilinganishwa na wafanyabiashara Mia nne waliokuwa kwenye soko la awali. 

Manufaa mengine ya Mradi ni kuwezesha halmashauri kupata mapato ya shilingi billioni 3.5 kwa mwaka pamoja na kukuza biashara katika Jiji la mwanza. 

Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya nyamagana Amina Makilagi amesema katika kipindi cha miaka mitatu cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan,wilaya hiyo imepokea billioni 350 kutoka serikali kuu ambazo zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya kimkakati ya Meli ya Mv.Mwanza hapa kazi tu,Upanuzi wa bandari ya mwanza kaskazini pamoja na mradi wa chanzo ya maji Butimba. 

Naye Mbunge wa Jimbo la nyamagana Stanslaus Mabula amemshukuru Rais Samia kwa kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii wananchi wilaya nyamagana. 

"Mradi wa ujenzi wa soko kuu la mwanza ulianza wakati wa serikali ya awamu ya nne na katika kipindi hicho ulikuwa unatekelezwa kwa kusuasua lakini katika miaka mitatu ya Mama Samia ameutoa kwenye hatua ya msingi mpaka kufikia hatua hii ya umaliziaji na hilo limewezekana baada ya serikali ya awamu ya Sita kutoa zaidi ya billioni 20 kwa ajili kutekeleza mradi huu muhimu Sana kwa maendeleo ya biashara katika Jiji letu"alisema Mabula









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top