Na Angela Sebastatian- Bukoba
MAHAKAMA ya hakimu mkazi Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera imefunga rasmi mwenendo kabidhi kuhusu shauri namba 17740 linalowakabiri washitakiwa tisa akiwemo padri wa kanisa Katoliki pamoja na baba mzazi wa mtoto Noela Asimwe Novart (2.5) ambaye aliuawa na kisha kukatwa mikono yako na mwili kutelekezwa katika karavati.
Waziri Magumbo mwendesha mashitaka wa mkoa wa Kagera kwa kushirikiana wa mawakili wenzake wanne wa serikali akiwemo Erick Mabagala alisema kuwa kesi hiyo ilifikishwa mbele ya hakimu Mkazi mfawidhi mahakama ya wilaya Bukoba Elipokea Yona kwa mara ya kwanza Juni 28 mwaka.
Amesema Mei 30 mwaka huu mtoto Noela aliibwa na watu wasiojulikama ambao walifika nyumbani kwao marehemu huyo na kumpola mikononi mwa mama yake kisha kutokomea kusikojulikana ambapo Juni 17mwaka huu mwili wa Noela ulipatikana ukiwa umetelekezwa katika karavati lililoko barabara ya Ruhanga ukiwa umekatwa mikono.
Magumbo akisaidiana mawakili wanne wa Jamhuri walisoma maelezo yaliyotolewa na mashaidi 52 na kisha kutoe vielelezo 37 ambapo 27 nyaraka na vielelezo kumi vya kushikika ikiwemo mifupa miwili marehemu Noela mbele ya mahakama hiyo.
Amesema kilichokuwa kinafanyika tangu shauri hilo kufikishwa mahakamani hapo ni kujilidhisha chini ya kifungu cha sheria 246 ya mwenendo wa makosa ya jinai ambapo upelelezi ukikamilika ,washtakiwa wanatakiwa kusomewa ushahidi na mashahidi watakaowasilishwa wakati wa kesi baada ya kupelekwa mahakama kuu yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Amewataja washtakiwa wanaokabiliwa na shitaka hilo ni Elpidius Rwegoshora padri wa Jimbo Katoliki la Bukoba ambaye ni mshtakiwa namba moja na Novath Venant baba mzazi wa mtoto Noela Washtakiwa Nurdin Masoud, Ramadhan Selestine, Rwenyagila Alphonce, Dastan Burchard, Faswiu Athuman, Gozibath Archard na Dezdery Everigist.
Kwa upande wake hakimu Yona amesema mahakama hiyo imefunga kabidhi mwenendo wa shauri hilo la kosa la mauaji linalowakabiri washitakiwa tisa na inapelekwa mahakama kuu kanda ya Bukoba na hakutaja tarehe nyingine ya kusikilizwa kesi hiyo ambapo alidai wanasubiri maelekezo ya mahakama kuu hivyo washitakiwa watajulishwa.
Washtakiwa wote tisa leo wamesimama peke yao baada ya hakimu kuwauliza kama wanajambo la kueleza ambapo mshitakiwa nammba moja Elpidius Rwegoshora ,namba mbili. NovathVenant,tatu Nurdin Masud,tano RwenyagiraAlfonce,saba Dunstan Burchard ,nane Gozbart Arikad na Dezideri Everigist namba tisa walisema wataleta mashaidi wakati kesi yao itakapoanza kusikilizwa huku mshtakiwa namba nne na sita hawana mashaidi ingawa mshtakiwa namba moja anatetewa na mawakili wawili ambao Mathias Rweyemamu na Pontian Mujuni.