CCM Mara Yaridhishwa na Utendaji Kazi wa Tanroads Mkoa Katika Utekelezaji na Usimamizi wa Miradi ya Barabara

GEORGE MARATO TV
0

 

Na Shomari Binda-Musoma 

CHAMA cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mara kimedai kuridhishwa na utendaji kazi, utekelezaji na ufatiliaji miradi ya barabara inayofanywa na Wakala wa Barabara Tanroads mkoa wa Mara.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Mara Ibrahim Mjanakheri  alipokuwa akizungumza na George Marato TV kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake.

Amesema serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan, imefanya kazi kubwa kuleta fedha za miradi ya maendeleo na mkoa wa Mara umenufaika.

Katibu huyo amesema eneo la miundombinu ikiwemo ya barabara imepata fedha na Tanrods mkoa wa Mara imefanya kazi nzuri katika kusimamia na miradi inaendelea vizuri.

Amesema katika kipindi cha mvua barabara zote zilikuwa zikipitika na hakuna taarifa yoyote iliyolipotiwa ya barabara kushindwa kupitika kwa kukatika

Mjanakheri amesema hali hiyo ni kuonyesha Tanrods mkoa wa Mara inatekeleza vizuri majukumu yake kupitia usimamizi wa meneja wa mkoa mhandisi Vedastus Maribe na wasaidizi wake.

Amesema ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya Makutano Juu-Nyamswa-Ikoma Geti kilometa 135 ujenzi sehemu ya pili ya Sanzate-Natta kilometa 40 wenye thamani Zaidi  ya shilingi bilioni  39.46 unaendelea kusimamiwa vizuri.

Amesema kwenye mradi huo mkandarasi na serikali Zaidi ya shilingi bilioni 5.04 na kuomba wasimamizi wa masuala ya kibajeti kuiongezea fedha Tanrods mkoa wa Mara ili iweze kukamilisha miradi kwa wakati.

" Kwa mkoa wa Mara ipo miradi mingi ambayo inaendelea na kwa upande wa barabara inatekelezwa vizuri chini ya usimamizi wa Tanrods mkoa wa Mara.

Kwa dhati tunampongeza meneja wa Tanrods mkoa wa Mara na timu yake kwa kazi wanayoifanya na wanaenda vizuri kikubwa waongezewe kasi ya kupewa fedha ya ukamilishaji"Amesema

Katibu huyo wa CCM mkoa wa Mara ameishukuru serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi mkoa wa Mara kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top