Askari Kata ya Kamnyonge Boniphace Lazaro Asisitiza Nidhamu Mashindano ya Polisi Jamii Cup Musoma 2024

GEORGE MARATO TV
0


Na Shomari Binda-Musoma

WACHEZAJI wanaoshiriki mashindano ya Polisi Jamii Cup Musoma 2024 wametakiwa kuzingatia nidhamu ili kulinda vipaji vyao.

Ujumbe huo umetolewa Septemba 17 na askari Kata wa Kata ya Kamnyonge Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Boniphace Lazaro kwenye mchezo kati ya Lake Victoria na Kamnyonge.

Amesema nidhamu ndio njia ya kuweza kufika kwenye mafanikio ya kimichezo kwa mchezaji yoyote.

 Lazaro amesema mchezaji yoyote mwenye kipaji kisha akazingatia nidhamu ni rahisi kupata mafanikio na kufika mbali na Kila mchezaji kulinda usalama wa mchezaji mwenzake kutokuumizana.

" Tuzingatie nidhamu tunapokuwa uwanjani ili kuvilinda vipaji vyenu na ndio njia itakayowawezesha kufika mbali.

Kupitia mashindano haya pia tunapeana elimu ya kuzuia uhalifu kwa kutoa taarifa tufanye  hivyo kwenye Kata zetu kupitia polisi Kata",amesema.


Katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Mara sekondari timu ya Lake Victoria imechomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kamnyonge fc.

Mashindano hayo ya Polisi Jamii Cup Musoma 2024 yataendelea tena Leo kwa mchezo kati ya Ajax fc na Mshikamano

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top