WAZIRI Mkuu Mh Kassim Majaliwa amekutana na kuzungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ndanda iliyopo Wilaya ya Masasi na Shule ya Msingi Nachingwea iliyopo Wilaya ya Nachingwea.
Wanafunzi hao ambao wako wilayani Nachingwea kwa ajili ya ziara ya kitaaluma ikihusisha ufanyaji wa mitihani ya kujipima ya ujirani mwema.
Wakiwa uwanja wa ndege wa Nachingwea kwa ajili ya Kujifunza majukumu ya uwanja wa ndege,wanafunzi hao wameta fursa hiyo ya kumpokea na kuzungumza na waziri mkuu katika maeneo hayo.
Waziri mkuu Majaliwa amewasili Wilayani Nachingwea akielekea wilayani Ruangwa ambapo atakuwa mgeni Rasmi katika harambee ya Kanisa Katoliki jimbo la Lindi.
Harambee hiyo kwa ajili ya Maandalizi ya Jubilei na ujenzi wa kanisa jipya la jimbo katoliki Lindi inayafanyika leo Julai 27, 2024 wilayani Ruangwa.

.jpg)



Comments
Post a Comment