MJANAKHERI APONGEZA KASI YA MAENDELEO KISIWA CHA RUKUBA KIKITIMIZA MIAKA 50

GEORGE MARATO TV
0

MJANAKHERI APONGEZA KASI YA MAENDELEO KISIWA CHA RUKUBA KIKITIMIZA MIAKA 50

Na Shomari Binda-Musoma

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) mkoa was Mara Ibrahim Mjanakheri amepongeza kasi ya maendeleo inayofanywa Kisiwa cha Rukuba.

Kisiwa cha Rukuba kilichopo jimbo la Musoma vijijini kilianzishwa mwaka 1974 na mwaka huu wa 2024 kinatimiza miaka 50

Akiwa Kisiwani hapo na jana septemba 11 na msafara wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa Fadhili Maganya Katibu huyo wa CCM amesema kasi ya maendeleo ikisukumwa na mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo inapaswa kupongezwa.

Amesema Profesa Muhongo mchango wake ni mkubwa katika kuhamasisha maendeleo ya kisiwa hicho ikiwa ni pamoja na kwenye elimu na afya.

Mjanakheri amesema bila uhamasishaji katika eneo lolote maendeleo hayawezi kupatikana na harambee zinazofanywa na mbunge Muhongo maeneo mbalimbali zimekuwa zikisaidia

" Maendeleo ya kisiwa cha Rukuba ni ya kasi na yanapita maeneo mengine na hii ni kazi kubwa inayofanywa na serikali mbunge wa jimbo pamoja na wananchi",amesema.

Kisiwa cha Rukuba kilitambuliwa na kupewa hadhi ya kijiji Mwaka 1974 kikiwa nimoja ya vijiji vinne (4) vya Kata ya Etaro pamoja na Busamba, Etaro na Mmahare.

Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya mbunge wa jimbo hilo inasema baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka 50 ya Kisiwa cha Rukuba ni kuwepo kwa shule ya msingi yenye vyumba vya madarasa vya kutosha na madawati ya kutosha. 

 Shule ina ofisi mbili (2) za walimu,mwalimu mkuu maktaba ya shule ya msingi na kila mwalimu wa shule ya msingi kupewa nyumba ya kuishi ya shule

Aidha Kisiwa hicho kina kituo cha afya kipya (Zahanati imepanuliwa na kuwa Kituo cha Afya) shilingi milioni 500 zikitolewa kwenye ujenzi na shilingi milioni 100 za vifaa tiba

"Umemejua (solar) kutumiwa na baadhi ya wakazi wa hapo Kisiwani kampuni binafsi inauza umemejua.

"Miradi mipya inayotekelezwas sekondari inajengwa kwa nguvu za wananchi na viongozi wa,umemejua unafungwa kwenye kituo cha afya na ni mradi wa REA wa shilingi milioni 345", ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Pia tàarifa hiyo ya ofisi ya mbunge imesema RUWASA itafunga miundombinu ya usambazaji wa maji safi na salama baada ya kuwepo umemejua mwingi na wenye uwezo mkubwa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top