Ujenzi wa barabara za lami kukuza uchumi wa wananchi Tanganyika

GEORGE MARATO TV
0


Tanganyika - Katavi

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2025 Ndugu Ismail Ali Ussi, ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Mkoa wa Katavi kwa kutekeleza ujenzi wa barabara za kiwango cha lami za Mji wa Majalila Wilaya ya Tanganyika Mkoani humo zenye urefu wa km 4.0 huku zikitajwa kuwa chachu ya ustawi wa maendeleo ya watu  kiuchumi na Kijamii.

Ussi amezungumza hayo mara baada ya kuzindua barabara hizo na kuongeza kuwa utekelezaji makini wa majukumu ya TARURA  utawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi kutokana na unafuu utakaokuwepo kutokana na kuimarika kwa miundombinu ya usafirishaji  hivyo kila mmoja atanufaika na ukuaji wa uchumi.

Awali akisoma taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 Ismail Ali Ussi, Meneja wa TARURA Wilaya ya Tanganyika Mhandisi. Nolasco Kamasho amesema mradi  wa barabara  za Mji wa Majalila uliojengwa Kijiji cha Majalila Kata ya Tongwe una urefu wa km 4.0 na umegharimu zaidi ya  shilingi bilioni 1.862 

Mhandisi huyo amesema  utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa barabara hizo unatokana na fedha za Mfuko wa Barabara, hivyo kama TARURA walikuwa na jukumu la kuhakikisha ujenzi wa barabara unakamilika kwa wakati na ukiendana na thamani  halisi ya fedha. 

Aidha, mkazi wa Mji wa Majalila Maria Shija amesema barabara hizo zitawasaidia kufika kwa haraka katika  huduma za kijamii kama vile   vituo vya afya na kuondoa adha ya usafirishaji wa mazao na bidhaa mbalimbali kutoka mashambani na kuyafikisha kwenye masoko. 




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top