Ccm Mkoa wa Tanga Yatoa Onyo Kwa Wanasiasa

GEORGE MARATO TV
0


 

Na MASHAKA MHANDO, Tanga 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga, kimewataka wanasiasa watakaoingia mkoa huo kufanya siasa, watumie matamshi yasiyokuwa na uvunjifu wa amani ili Taifa liendelee kuwa na Amani.

Akitoa salamu za Ed El Fitr kwa kuzungumza na waandishi wa Habari machi 29 mwaka huu 2025, Mwenyekiti wa CCM mkoani Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu (MCC) Rajab Abdarahman alisema kuwa mkoa wa Tanga umekuwa ukitumia hekima na busara katika kulinda Amani hivyo watu wengine wasijaribu kuvuruga Amani hiyo.

Alisema wanasiasa watakaofika eneo la Manga mpakani mwa Tanga na mkoa wa Pwani wajue wanaingia mkoa ambao amani inalindwa kama ambavyo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akihubiri kuhusiana na masuala ya amani.

"Wale watu waliojipanga kwa ajili ya kufanya siasa zenye viashiria vya kuvunja amani, hatutamuonea haya, waje kwa adabu watakapoingia kule Manga (mpaka wa Tanga na Pwani) vinginevyo hatutawavumilia, Tanga kipaumbele chetu ni kulinda amani.," alisema akiwaasa wanasiasa.

Alisema Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batlida Salha Burian na Kamati yake ya Usalama ya Mkoa, wamekuwa wakitumia busara na hekima kuhakikisha amani inadumishwa katika mkoa huo hivyo si busara kuwachokoza viongozi hao.

Mwenyekiti huyo pia alitumia nafasi hiyo kuwaasa waumini wa dini ya Kiislamu kuwa na mwenendo mzuri hata baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema kumaliza Ramadhani kisha mtu akarejea kwenye maasi si tabia njema na funga yake yote itakuwa kazi bure hivyo akawataka waendelee kumcha Mungu na kutenda yaliyo mema.

Pia mwenyekiti aliwashukuru wafanyabiashara wa chakula kwa kuuza bidhaa zao bei za kawaida tofauti na miaka mitatu iliyopita walikuwa wakipandisha bei Kila ifikapo mwezi wa Ramadhani.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top