Polisi Mwanza yaendeleza Elimu Visiwani Kukomesha Uhalifu

GEORGE MARATO TV
0


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeendea kutoa elimu na kuimarisha hali ya ulinzi kwenye visiwa vya Yozu, Nyamango, Chembaya, Soswa, Zelagula Gembale na Kasalazi Halmashauri ya Buchosa wilaya ya Sengerema mkoani humo.

Akizungumza na wakazi wa Kisiwa cha Yozu, leo Jumamosi, Januari 18.2025 Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Lwelwe Mpina amewataka wananchi kutojihusisha na uhalifu wa kuiba mazao uvuvi sambamba na kuacha uvuvi haramu.

Aidha, ACP Mpina amewataka wananchi wa visiwa hivyo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kufichua wahalifu wanaojificha kwenye visiwa hivyo.

Kwa upande wao, wakazi visiwa hivyo, wamepongeza jitihada zinazofanywa na Jeshi  la Polisi za kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli za maendeleo bila kuwa na hofu yoyote ya kiusalama.





*Kutoka Dawati la Habari Polisi Mwanza*

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top