Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika Jijiji Dodoma leo January 19,2025 umepitisha kwa asilimia 100 jina la Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ndiye atakayegombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi wa mwaka huu 2025.
Rais Samia amepata kura zote za ndio 1924 (100%) zilizopigwa na Wajumbe ambapo hakuna hata Mjumbe mmoja aliyesema hapana.