WAZIRI wa ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa JKT Mh Dkt Stergomena Tax,amesema jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania,litaendelea na majukumu yake, lakini pia litashiriki kikamilifu katika kudumisha mila na tamaduni zenye kuleta taifa pamoja.
Mh Tax,ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mashindano ya utamaduni ya mkuu wa majeshi ambayo yamefanyika Msasani Club na kushirikisha vikundi tisa vya ngoma za asili na bendi kumi za muziki wa dansi.
Pamoja na kumpongeza mkuu wa majeshi ya ulinzi jenerali Jacob John Mkunda, kuanzisha wazo la kuanzishwa kwa mashindano hayo amesema yatasadia kuleta mabadiliko makubwa ndani ya jamii.
Amesema kazi hiyo ambayo imefanywa na jeshi,kupitia mkuu wa majeshi ni sehemu ya kuunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na amri jeshi mkuu Rais Dr Samia Suluhu Hassan,kwa kuweka nguvu kubwa za
kuendelezwa,kudumisha na kuzienzi mila na desturi za kitanzania.
Naye mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini jenerali JACOBO JOHN MKUNDA,amesema mashindano hayo yamekuwa na mafanikio makubwa, na kusema jeshi litaendelea kufanya mashindano hayo kila mwaka katika kudumisha utamaduni.
Mkuu huyo wa majeshi ya ulinzi,amesema hivi sasa baadhi ya tamaduni zimeanza kutoweka hivyo jeshi lina wajibu pia kushiriki katika kuhuisha tamaduni hizo
Mashindano hayo yameshirikisha vikundi tisa vya ngoma za asili na bendi kumi za muziki wa dansi,ambapo vikundi vya ngoma na muziki wa dansi,kutoka Mlale JKT, TMA,Makotopola na Mwenge Jazz.
Vingine ni Mgulani JKT,Mbweni JKT na Nyuki kutoka Zanzibar vikiibuka vinara katika mashindano hayo kupewa zawadi mbalimbali