Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya akutana na Rais Museveni

GEORGE MARATO TV
0



_ ▪️Asema Serikali itaimarisha vitengo vya tathmini na utekelezaji wa wizara _

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuboresha elimu wakati ikitekeleza mtaala mpya wa elimu ili kuziba mahitaji ya shuleni.

“Kwa kuwa tunaenda katika mtaala mpya wa elimu, tutaendelea kuboresha matumizi Tutaendelea kuboresha gharama kwa mahitaji yanaongezeka kila wakati katika kumfanya mtoto asome vizuri,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma, leo (Alhamisi, Aprili 9, 2026) wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea, Agnesta Lambert Kaiza, kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa Waziri Mkuu ambaye alitaka kujua kauli ya Serikali juu ya kukomesha michango inayotozwa shuleni.

Dkt. Mwigulu amesema Serikali haina shida na chakula cha chakula ambacho imekuwa ikitolewa shuleni lakini akasisitiza kuwa endapo kutokea michango mingine yoyote, ni lazima ifuate miongozo ya serikali na ipate baraka za Wakuu wa Mikoa husika.

Akitoa mfano wa mchango ambao haukubaliki, Waziri Mkuu amesema akiwa ziarani mkoani Katavi, alipokea malalamiko ya Mama mmoja ambaye mwanaye alizuiwa kujiunga na shule ya sekondari hadi atoe sh. 50,000/- ya dawa.

“Nilielekeza yule mtoto arudishwe shuleni na nimpongeze Mkuu wa Mkoa ambaye amenijulisha kuwa yule mtoto amesharudi shuleni.

Mbali na changamoto hiyo, Waziri Mkuu amewapongeza walimu nchini kwa kujitoa bila kuchoka ili kusaidia watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora. "Sote tunatambua kuwa walimu wengi wamejitoa sana katika baadhi ya maeneo. Licha ya wingi watoto na uchache wa walimu, kwa juhudi zao wamehakikisha wanakamilisha silabasi zao ili watoto wetu wapate bora."

Akielezea kuhusu uwepo wa walimu wa kujitolea katika baadhi ya shule, Waziri Mkuu amesema alishatoa maelekezo kwamba malipo ya walimu wa aina hiyo yatoke kwenye suala la ndani ya Halmashauri husika badala ya kuwataka wazazi wachangie malipo yao.

“Wazo la kuwa na walimu wa kujitolea ni jema, na sisi wakati tunasoma tulipata mafunzo ya ziada (tuition) kwa walimu wa aina hii. Wazo la kuwa na walimu wanaojitolea ni jema lakini malipo yao yasilipwe na wazazi, badala ya kwenda kwenye michango, Mamlaka za Serikali za Mitaa watumie kutuma ya ndani.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali itafanya vitengo vya tathmini na utaendelea katika kila wizara ili kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. “Kwenye kila wizara, kuna hivi vitengo vya uchanganuzi na tathmini. Tunapanga kuongeza fedha zao ili kutimiza wajibu wao katika miradi na shughuli zote za Serikali.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Monduli, Isack Joseph Copriano aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kuimarisha timu ya tathmini na ufanisi ili kuharakisha majibu ya wananchi na hususan kero zao.

Alisema katika kuimarisha mawasiliano na wananchi, Serikali imeanzisha kituo cha kupokea simu (Call Centre) yenye namba 190 ambapo mwananchi mwenye shida yoyote anaweza kupiga simu na kutoa kero yake na kwamba atajulishwa majibu yake kupitia kituo hicho.

Amesema Serikali inataka utaratibu wa kila kiongozi kubeba hoja za wananchi kupitia rejesta ambazo zitakuwa zinatumika kwenye ofisi za viongozi kurekodi kero za wananchi na kutoa mrejesho serikalini kila mwisho wa mwezi.

“Utaratibu wa kupokea kero siyo wa kwenye ziara tu, kila viongozi watapaswa kutoa taarifa ya idadi ya wananchi waliowahudumia na majibu waliyoyapa wakionesha hoja zipi walipokea, namba za simu za wananchi waliohudumiwa na hizo hoja zimetatuliwa vipi.”

“Tunataka utaratibu wa kiongozi kubeba hoja za wananchi na siyo kuacha wananchi waende kutafuta wajumbe kwa viongozi,” alisisitiza.

* (mwisho) *


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top