Mbunge Angela Kizigha Ateuliwa Mshauri wa Rais Masuala ya Kijamii

GEORGE MARATO TV
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali ambapo katika mkeka wake wa Ijumaa hii amemteua Mbunge wa kuteuliwa, Mhe. Angela Charles Kizigha kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Jamii kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 24, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka

Itakumbukwa kuwa tarehe 20 Aprili, 2026, Mhe. Angela Charles Kizigha aliteuliwa kuwa Mbunge ambapo tarehe 09 Aprili, 2026, aliapishwa rasmi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, uteuzi huo unalenga kuimarisha ushauri wa kisera katika masuala ya kijamii yanayogusa ustawi wa wananchi.

Mhe. Angela Kizigha anatarajiwa kusaidia katika kuratibu na kushauri kuhusu programu na mikakati ya kijamii, ikiwemo maendeleo ya jamii na ustawi wa makundi mbalimbali.

Uteuzi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha utendaji kazi katika ngazi ya juu ya maamuzi ya Sera.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top