Uboreshaji Miundombinu ya Elimu Umeongeza Chachu ya Ufaulu Kwa Wanafunzi

GEORGE MARATO TV
0


Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma.

MHANDISI mwandamizi wa sekta ya ujenzi Magesa Mwita amewaeleza walimu,wazazi na wanafunzi dhamira ya serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule iliyopelekea kuongeza chachu ya ufaulu kwa wanafunzi.

Amesema uwepo wa mazingira salama ya kujifunzia yamewezesha wazazi wengi kupeleka watoto wao shule kwa wingi.

Ameyasema hayo kwenye maafari ya wanafunzi wa kidato nne  shule ya sekondari Murembe iliyopo Kata ya Bweli Manispaa ya Musoma mkoani Mara wakati wa hotuba yake akiwa ndie mgeni rasmi wa shughuli hiyo.

Amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha kila mtoto anajifunza katika mazingira salama yenye miundombinu bora kwa kutenga fedha na kuboresha madarasa,mabweni na maabara katika shule mbalimbali hapa nchini.

Aidha ameipongeza bodi, uongozi wa shule hiyo na kamati ya ujenzi kwa kusimamia vema fedha za ujenzi wa miundombinu iliyotolewa na serikali kuendelea kuboresha mazingira ya Elimu.

Hata hivyo mhandisi Magesa hakusita kuwapongeza wahitimu hao wa kidato cha nne na kuwaasa kuzingatia maadili,bidii na nidhamu ili kuwawezesha kufanikisha safari yao kielimu huku akiwasisitiza uwajibikaji na kujituma kwenye kilimo, ufugaji,ufundi na ujasiriamali pindi watakapohitimu kuweza kujiajiri  na kutojihusisha na vitendo viovu pindi watakaporudi majumbani mwao.

"Bidii za ufundishaji kwa walimu wa shule hii imewezesha kuwepo kwa ongezeko la ufaulu mzuri katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ni dhahiri uwajibikaji bora wa wasimamizi wa elimu,"amesema Magesa.

Sanjari na hayo amewakumbusha kumtanguliza Mungu kuwasaidia katika mitihani yao ya kuhitimu  Elimu ya sekondari.

Amehitimisha hotuba yake kwa kuukabidhi uongozi wa shule hiyo luninga ya nchi 43 na king'amuzi lengo kuwezesha walimu kupata taarifa mbalimbali.



         

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top