Vijana Watakiwa Kutunza Mazingira, Amani ya Jamii

GEORGE MARATO TV
0


*Na:Dawati la Habari Polisi Mwanza*

Mkuu wa Kituo cha Polisi Nyegezi, Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Aziza Msangi ameitaka jamii hasa vijana kutunza mazingira na kudumisha amani kwa manufaa yao na vizazi vijavyo.

Wito huo umetolewa Septemba 19, 2025 na ASP AZIZA kwa kushirikiana na Taasisi ya Jane Goodall kupitia mpango wa Roots & Shoots, katika kituo cha Polisi Nyegezi, walipokutana na wanafunzi kutoka shule ya Sekondari Twihulumile, waliotembelea kituo hicho kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo ulinzi wa mazingira, haki za wanyama na amani ya jamii, kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani yanayofanyika kila mwaka ifikapo Septemba 21.

Katika mafunzo hayo, ASP Aziza aliwasilisha mada mbalimbali ikiwemo: Nafasi ya vijana katika kudumisha amani na usalama wa jamii, Umuhimu wa kutunza mazingira na wanyama pori, Maana na kazi ya Dawati la jinsia na watoto, aina na ukatili wa kijinsia na jinsi ya kujiepusha na makundi hatarishi na vitendo vya uhalifu pamoja na Ushirikiano kati ya jamii na vyombo vya dola katika kuimarisha ulinzi na Usalama.

Elimu hiyo iliambatana na zoezi la upandaji miti ya matunda na ya kivuli katika eneo la kituo, kama ishara ya kuenzi amani na kuhamasisha utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wao viongozi wa Taasisi ya Jane Goodall na wanafunzi walimpongeza ASP Aziza kwa elimu waliyopata na kuahidi kuwa mabalozi wa amani na mazingira katika jamii zao.

Huo ni mwendelezo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kushirikiana na taasisi mbalimbali kuimarisha usalama wa kijamii, kudhibiti vitendo vya ukatili na kujenga jamii endelevu yenye mshikamano.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top