Dondoo za Hotuba ya Ndg. Anthony Mavunde akihutubia maelfu ya Wananchi wa Kata ya Ngh’ongh’ona tarehe 26.09.2025
▪️Pongezi kwa Dkt. Samia S. Hassan kwa mageuzi makubwa ya sekta ya Afya,Elimu,Maji,Barabara na Nishati.
▪️Ujenzi wa Kituo cha Afya Ngh’ongh’ona.
▪️Ukamilishwaji na kusajiliwa Shule ya Sekondari Mapinduzi.
▪️Upimaji na Umilikishwaji wa Ardhi kwa wananchi wa Ngh’ongh’ona.
▪️Uchimbwaji Kisima na kuongeza kina cha bwawa la Umwagiliaji.
▪️Ujenzi wa Soko na Stendi ya Mabasi.
▪️Ukamilishwaji usambazaji nishati ya umeme maeneo yaliyobaki.
▪️Ununuzi wa Mtambo(Motor Grader) kwa ajili ya Jimbo la Mtumba ili kusafisha na kufungua barabara.
▪️Uanzishwaji wa viwanda vidogo kupitia 10% ya mikopo ya wakinamama,Vijana na watu wenye ulemavu.
▪️Uanzishwaji wa Klabu za wazee za Kata.
▪️Uchimbaji visima vya Maji safi eneo la Mhande na Kwa Mjeni.
▪️Ukamilishwaji wa Zahanati ya Mapinduzi B.
▪️Utatuzi wa mgogoro wa Ardhi Itumbi na Mapinduzi B.
▪️Ulipwaji wa Fidia wananchi waliopisha ujenzi wa Barabara ya Ntyuka-Mvumi-Kikombo.
▪️Uanzishwaji wa MAVUNDE CUP kata ya Ngh’ongh’ona.
▪️Ununuzi wa mtambo mkubwa wa kudurufu mitihani(𝙋𝙝𝙤𝙩𝙤𝙘𝙤𝙥𝙞𝙚𝙧 𝙈𝙖𝙘𝙝𝙞𝙣𝙚𝙨) kwa kila kata.
▪️Ujenzi wa vivuko vya watembea kwa miguu na magari.
▪️Ukarabati mkubwa wa Barabara ya Ngh’ongh’ona-Mapinduzi-Chololo.