Mapokezi Ya Dk.Nchimbi Ndani ya Jimbo la Kisesa, Meatu Akiendelea na Mikutano Kuomba Kura Kuelekea Uchaguzi Mkuu

GEORGE MARATO TV
0


MAMIA ya Wananchi  wa Kata ya Mwandoya ndani ya Jimbo la Kisesa,wilayani Meatu wakimsikiliza  Mgombea Mwenza wa Urais wa   Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi  wakati akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara leo Septemba 2,2025,wakati akiendelea na Mikutano yake ya Kampeni mkoani Simiyu.

Katika mkutano huo wa kampeni,Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi alimnadi Mbunge wa Jimbo hilo la Kisesa,Musa Godfrey Mbuga pamoja na diwani wa kata ya Lubiga,Juma Mpina ambaye ni kaka wa mbunge wa zamani wa jimbo laKisesa, Luaga Mpina. 

Pamoja na mambo mengine Balozi Dkt.Emmeanuel Nchimbi amekuwa akiinadi Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia Suluhu,Mgombea mwenza wa Urais,wabunge na madiwani wa Chama hicho.









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top