Mgombea Ubunge Jimbo la Rorya Mh Jafari Wambura Chege amewaambia wananchi wa Bukura waliojitokeza kwa wingi,kwamba wajitokeze kwa wingi Tarehe 29/10/2025 Kwenye Vituo vya Kupigia Kura.
Amewaeleza kujitokeza kwao kwa Uwingi na Kupiga kura kwa Dr Samia Suluhu Hassan kutarahisisha ukamilifu wa One stop border ya Kirongwe,ambayo ukamilifu wake itaongeza Uchumi wa familia, Mapato ya halmashauri,upanuzi wa Eneo lao kwa kuzingatia utazamiaji wa Mnada Mkubwa wa Mifugo(Ng'ombe).
Ndugu wananchi wa Bukura Miradi ya kimkakati ikiwemo Barabara ya Lami kufika Kirongwe kunahitajika sisi kujitokeza kwa wingi kumpigia *Dr Samia* Kura ili kutupa Ujasiri wa kwenda mbele zake.
Natamani nitambe kwa Uwingi wa Kura zenu kwa Mafiga 3,ili tukamilishe Mradi wa Maji Thabache kwa ajili Yenu,pamoja na Barabara za kuwaunganisha ikiwemo la Bwiri to Kyariko na hata hii ya Lwanda Agago.