*Serengeti, Mara –
Mbunge Mteule wa Viti Maalum Mkoa wa Mara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mh. Agnes Marwa, amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Serengeti kushiriki uzinduzi wa kampeni za uchaguzi kwa Jimbo hilo, hafla ambayo mgeni rasmi ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Comrade Mohammed Kawaida.
Katika picha akiwa na wanawake wa Wilaya ya Serengeti kwa lengo la kuwaelekeza na kuwahamasisha kuhusu mpango kazi wa kusaka kura kwa kila kata, ili kuhakikisha ushindi wa CCM kuanzia ngazi ya Rais, Wabunge hadi Madiwani katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza na wanawake hao, amesisitiza kuwa maendeleo ya Taifa yana msingi imara kupitia uongozi wa CCM, na kwamba ni jukumu la kila mwanachama na hasa wanawake, kuhakikisha wanafanya kazi ya kisiasa kwa bidii ili chama hicho kiendelee kuongoza dola.



