*Tarime Mjini, Mara – 20 Septemba 2025*
Mbunge Mteule wa Viti Maalum Mkoa wa Mara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Agnes Marwa, leo ameshiriki katika uzinduzi wa kampeni za udiwani Kata ya Nyandoto, Tarime Mjini, ambapo alimnadi Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Samia Suluhu Hassan na pia Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Ndg. Esther Matiko*, pamoja na *Mgombea wa Udiwani Kata ya Nyandoto, Ndg. Doris Chacha*.
Akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika eneo la *Gamasala*, Agnes Marwa alisema kuwa *Esther Matiko* ni miongoni mwa wanasiasa wachache waliobobea katika kujenga hoja bungeni na ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wananchi wa Tarime hata kabla ya kujiunga na CCM.
Akimnadi amesema Uamuzi wake wa kurudi CCM ni wa busara na umekuja kwa wakati sahihi. Anaelewa changamoto za wananchi wa Tarime na ana uwezo wa kuzisimamia ipasavyo kupitia jukwaa la Bunge kwa kushirikiana na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Agnes Marwa amehitimisha kwa kuwaomba wakazi wa Nyandoto na Tarime Mjini kwa ujumla kuhakikisha ifikapo *Oktoba 29*, wanachagua wagombea wa CCM katika ngazi zote — *Rais, Mbunge na Diwani* — ili kuendeleza sera na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.