Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 23 Aprili, 2025 ametia Saini tamko la Sheria Kuu 446 za Tanzania zililofanyiwa Urekebu toleo la Mwaka 2023.
Dkt. Samia ametia saini wakati wa hafla ya uzinduzi wa toleo la Sheria zilizofanyiwa Urekebu la Mwaka 2023 iliofanyika Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.
Zoezi la Urekebu wa Sheria ambazo zimezinduliwa, limefanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kutumia Rasilimali fedha za ndani na Wataalamu wa ndani.