Na Shomari binda-Musoma
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt.Emanuel Nchimbi ameagiza Wizara ya Fedha kutoa fedha kwaajili ya kukamilisha upanuzi wa uwanja wa ndege Musoma.
Agizo hilo amelitoa leo aprili 23,2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM mkoa mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi wa uwanja huo.
Amesema maendeleo ya uwanja huo chini ya TANROADS mkoa wa Mara na ufatiliaji wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara ni mazuri bali nguvu inapaswa kuongezwa ikiwemo ya kifedha.
Dkt.Nchimbi amesema tayari mita 1000 za uwanja huo zimekamilika na zinazotakiwa ni mita 1705 hivyo zilizobakia zikamilishwe ili uanze kufanya kazi kwa muda uliokusudiwa.
" Kazi inafanyika vizuri kwenye upanuzi wa uwanja wetu wa ndege wa Musoma na nimuagize Waziri Mwigulu kupitia Wizara ya fedha kutoa kiasi cha fedha kilichobaki ili kukamilisha uwanja huu.
" Uwanja huu ukikamilika shughuli za utalii zitafanyika na huduma nyingine zitaendelea na nipongeze kazi nzuri ambazo zimefanyika hadi sasa",amesema.
Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ameishukuru serikali ya awamu ya 6 chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya utekelezaji wa miradi ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege Musoma.
Amesema chini ya Chama cha Mapinduzi kazi kubwa imefanywa katika utekelezaji wa ilani ndani ya mkoa wa Mara na kuwapongeza pia wanachama wa chama hicho.
Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema uwanja huo ukikamilika na kuanza kutoa huduma itaboresha shughuli za kiuchumi.
Aidha amesema Musoma mjini haina viwanda na kumuomba Katibu Mkuu kusaidia kusukuma uanzishwaji wa viwanda ili kuwezesha wananchi kiuchumi.
Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya upanuzi wa uwanja huo alipoutembelea meneja wa uwanja wa TANROADS mkoa wa Mara Mhandisi Vedastus Maribe amesema kazi zinaendelea kufanywa za upanuzi huo na lengo ni kuhakikisha kufika mwezi septemba unakamilika na huduma zimaanza kutolewa kama ambavyo zimekusudiwa.
Katibu Mkuu Balozi Dkt.Emanuel Nchimbi ameendelea na ziara yake mkoani Mara katika kuangalia utekelezaji wa ilani na kuangalia shughuli za maendeleo na leo licha ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa uwanja wa ndege Musoma ametembelea pia hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere