MNEC Manguzo aendelea Kuigusa Jamii

GEORGE MARATO TV
0



  BUSWELU ILEMELA

🗓️ 21/4/2025

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (MNEC)Ndugu Leonard  Mahenda Maarufu Kwa Jina la Manguzo ameendelea kuigusa Jamii Kwa kutoa Viti Mwendo (Wheel Chair)  30 Kwa watoto wenye Ulemavu.

Viti hivyo vimetolewa kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Watoto wa Africa Orphanage kilichopo Busenga, Buswelu Ilemela Mwanza Tanzania.

Akisoma Risala Mkurugenzi Wa Taasisi ya Inuka Angaza  Eva Samara  amesema Lengo Lao ni kuhakikisha Wanapata Viti Mwendo 100 kila Mwaka.

Mahende ambaye pia ni Mkurugenzi Wa QWIHAYA INTERPRISES na MNEC Taifa amekuwa akiigusa Sana Sana Jamii ya watu wenye ulemavu  Kwa Kutoa Viti Mwendo 30 (Wheel Chair) na kufanya Jumla ya Viti Mwendo 36 kwenye Kituo hicho

Akijibu Risala ya Mkurugenzi Wa Kituo cha Inuka Uangaze MNEC Manguzo  amesema Kitendo cha kutoa Viti Mwendo 30 ni ishara ya kufufuka na Yesu Kristu kama agizo la Upendo lilitolewa na Bwana yetu Yesu Kristu.

Aidha MNEC MANGUZO ameomba watoto wengine kuwasaidia Wenzao kufika sehemu Mbalimbali Kwa kuwaendesha Kutoka Eneo Moja kwenda lingine.

MNEC Manguzo amesema Mungu akimuwezesha kufika tarehe 26/12/2025 Atatoa Viti Mwendo zaidi ya vile alivyotoa Siku ya Leo na Atatoa cherehani Kumi (10) Kwa ajili ya Wazazi wa watoto wenye mahitaji Maalumu ili kujitengenezea kipato cha Uhakika

Akiwa Kenya kituo hicho MNEC Manguzo Amempatia Sare za Shule pair Tatu, Viatu Vya Shule Pair Tatu na Kumpatia Bima ya Afya Ili kumudu Gharama za Matibabu Mtoto Juma Pantaleo ambaye ni Mlemavu aliyeacha Shule Kwa Changamoto ya  Ulemavu na Sare za Shule pamoja na Kushindwa kumudu Gharama za Matibabu 

MNEC Manguzo alikuwa Mgeni rasmi kwenye Tukio la ESTER CHARITY 2025 Lililoandaliwa na CLOUDS MEDIA Chini ya Taasisi ya INUKA UANGAZE ORGANIZATION. 





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top