Ccm Mara Kugawa Kadi za Kielektroniki 6,45,000 Kwa Wanachama Wake Kuanzia Machi 29, 2025

GEORGE MARATO TV
0


Na Shomari Binda-Musoma

CHAMA cha Mapinduzi ( CCM) mkoa wa Mara kimepanga kugawa kadi za kielekronicki kwa wanachama wake 6,45,000 kuanzia machi 29.

KATIBU wa Siasa, Uenezi,Itikadi na Mafunzo Mkoa wa Mara Simon George Rubugu amesema kuwa Chama hicho kimepokea kadi za wanachama wa mkoa huo waliosajiliwa kwa mfumo wa  Kielektroniki zipatazo  645,000, ambapo kinatarajia kuanza zoezi la ugawaji wa kadi hizo.

Rubugu ameyasema hayo leo Machi 27,  2025, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake.

 Amesema kadi hizo zimebooreshwa kisasa  huku  akitoa  msisitizo kwa wanachama wa CCM  ambao bado hawajasaliliwa kujisajili kwani zoezi hilo ni endelevu. 

Kiongozi huyo amesema idadi ya kadi hizo  ni zaidi ya asilimia 51 ya makisio ya wapiga kura na zitasaidia kuwatambua wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya matawi, Kata, Wilaya hadi Mkoa kabla ya kuingia katika uchaguzi  unaotarajia kufanyika mwaka huu.

"Kadi hizi zitakuwa na faida kwa wanachama ikiwemo kuwatambua wanachama wote kwenye mfumo, urahisi wa kufanya nao mawasiliano, Mwanachama kuitumia kadi  katika matumizi ya miamala hivyo naomba wanachama wakati wanakwenda kuchukua kadi zao waende  na vitambulisho vyao vya NIDA au kadi ya mpiga kura kwa ajili ya kuingizwa kwenye mfumo.

"Tunashukuru sana juhudi thabiti zilizofanywa na Mwenyekiti wetu Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wanachama wanakuwa kwenye mfumo na haya ni mageuzi makubwa na mazuri sana kwa chama chetu ." amesema Rubugu.  

Pia amepongeza miradi ya maendeleo iliyofanywa na  serikali ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Rais Dkt.  Samia Suluhu  Hassan ikiwemo ujenzi wa miradi ya Kimkakati kama uwanja wa Ndege wa Musoma, Daraja la Magufuli  Mwanza, Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere,  miradi mbalimbali ya elimu, afya, barabara, maji ambayo amesema itakipa ushindi wa kishindo chama hicho kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.  

"Miradi ambayo imefanywa na serikali uhakika ni kwamba chama  kitashinda  kwa ushindi mkubwa sana, hii ndio reforms ya maendeleo miradi inaonekana kwa macho.  mkoa wa Mara tunao uwanja wa Ndege ambao utafungua fursa ya uchumi.   tunao mradi mkubwa wa maji wa Mugango-Kiabakari- Butiama huu umesaidia wananchi wengi na mradi mwingine wa maji  upo wa  Rorya unakwenda mpaka Tarime wa bilioni 134, wananchi wamekoshwa na miradi hii."ameongeza.

Aidha amewataka wanachama wa chama hicho mkoa wa Mara kuendelea kushikamana, kupendana na kuachana na makundi madogo madogo. Ili waendelee kuyasema kwa wananchi mema na maendeleo yote ambayo serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inayafanya maeneo mbalimbali hapa nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top