Na Shomari Binda-Musoma
MKURUGENZI wa hotel ya Le Grand Victoria ya mjini Musoma Ramadhani Msomi amewashukuru viongozi wa group la whasap la Jamii ya wana Musoma kwa kuendelea kuwaunganisha watu na kusaidiana kwenye matatizo.
Kauli hiyo ameitoa kwa niaba ya wana jamii hao walipokuwa wakikabidhi rambirambi ya msiba wa mama mzazi wa Selemani Keraba ambaye ni mmoja wa wana jamii ya Musoma.
Amesema kwa kipindi cha miaka 8 viongozi hao wamefanya kazi kubwa ambayo inapaswa kuungwa mkono na kuendelea kuifanya kazi hiyo.
Rama amesema sio kazi rahisi kuwasimamia watu na kukusanya michango yao na kusitokee lawama kwa kipindi chote na kudai wanaongozwa na uadilifu.
Amesema wanapaswa kuendelea kuwapa ushirikiano na kudai kwa upande wake ataendelea kutoa ushirikiano kwa kila jambo.
" Nikushukuru Mwenydkiti na viongozi wote wa group kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuwaunganisha watu wa Musoma.
" Sisi wakati mwingine tunakuwa nje ya Musoma lakini juhudi zenu mnakuwa mnatuunganisha pamoja lazima tuwashukuru",amesema.
Akikabidhi mchango kwa mfiwa kiasi cha shilingi milioni 3, 600,000 Mwenyekiti wa group la jamii ya wana Musoma Benedict Magiri amewashukuru wale wote waliochanga na kudai lengo ni kufanya makubwa zaidi licha ya kukabidhi fedha ya rambirambi kwa muhusika.
Amesema group lina lengo la kuwa na viti 500,tent 4 na vyombo vya matangazo na kukusudia kuanza kuvitafuta kwenye harambee itakayofanyika februari 21 na kuomba kila mwana umoja na wadau kuchangia kufanikisha hafla hiyo.
Akipokea rambirambi hiyo Selemani Keraba amewashukuru wana jamii ya Musoma kwa kumfariji wakatì wa msiba wa mama yake nz michango yao waliyoitoa.
Mweka hazina wa group hilo Ismail Massaro amesema utaratibu wa group kuhusu nichango na anayestahili kuchangiwa upo wazi ikiwa ni kuchangia misiba mitatu mfululizo.
Akizungumzia kuelekea hafla ya wana umoja itakayofanyia febrhari 21 amewakumbusha wana jamii kuchangia kabla ya mwisho wa mchango februari 15 kwa kuwa mchango huo ni sehemu ya vigezo vya kuweza kuchangiwa.