Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa shilingi Bilioni 40 kwa mwaka wa fedha2023/24 ili kuendelea kuimarisha miundombinu ya miradi mbalimbali ikiwemo ya Sekta ya Afya kwa kujenga Hospitali pamoja na vituo vya Afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ikiwa pamoja na Jimbo la Peramiho.
Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo Septemba 24, 2024 wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jimbo la Peramiho, Songea Mkoani Ruvuma.
"Kwa Mwaka wa fedha 2023/24 Serikali imetoa fedha kiasi cha Tsh: Bilioni 40 katika Jimbo la Peramiho ili kutekeleza miradi ya maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya kwa kujenga Hospitali pamoja na Vituo vya Afya." Amesema Waziri Mhagama
Aidha, Waziri Mhagama amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kufanya kazi na Hospitali ya St. Joseph's Mission ya Peramiho kama Hospitali ya Rufaa