Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa na Mlezi wa UVCCM Vyuo na Vyuo Vikuu Mohammed Ali Kawaida ameweka bayana msimamo wa Umoja wa Vijana wa CCM ya kuwa ifikapo 2025 UVCCM itasimama na Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa Zanzibar na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Tanzania
"Tunaona kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Serikali zote mbili, ifikapo 2025 Fomu ya Uraisi ni moja tu kwa Zanzibar ni Dkt Mwinyi na Bara ni Dkt Samia na katika hili hatutakuwa wanafiki tutasimama Imara kuyasema yote yaliyofanywa na Viongozi wetu"
Kawaida ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye Mahafali ya UVCCM Zanzibar yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Suza Tunguu Unguja Zanzibar tarehe 28 Septemba, 2024.
Aidha Kawaida amewahimiza vijana wote nchini kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukisemea kwa wananchi wote ili kiendelee kuaminika kwa wananchi na kuendelea kushika Dola. 8
Umoja wa Vijana wa CCM utafanya kazi usiku na mchana kusema mazuri yote yanayofanywa na Serikali zote mbili za mbilimbili za CCM