Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Tarime Rorya leo 22.09.2024 limefanya zoezi la kujaribu vitendea kazi vyake vyote vya kulinda raia na mali zao ili kujiweka tayari kwa lolote litakalojitokeza.
Vitendea kazi hivyo ikiwemo magari ya doria ya kawaida na magari ya maji washa, kikosi cha mbwa na farasi na kikosi vya Usalama barabarani na kikosi cha kuzuia ghasia vilionekana katika doria mitaa mbali mbali ya Mji wa Tarime ,Sirari na Rorya ili kuwaondoa hofu raia wema wanaofuata sheria na taratibu za nchi na kuwahakikishia kuwa ulinzi na usalama wao umeimarika.
Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime Rorya SACP Mark Njera amefanya ukaguzi wa vitendea kazi hivyo pamoja na ukakamavu wa askari kuhakikisha wepesi wao katika kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupongeza uimara wao uluotokana na mazoezi ya Utayari ya mara kwa mara.