Benki ya dunia yaipa kongole Misungwi kwa utekelezaji Mzuri wa miradi ya Boost na Sequip

GEORGE MARATO TV
0


Benki ya Dunia nchini imeeleza kuridhishwa na ubora wa miradi ya elimu iliyotekelezwa na Serikali wilayani misungwi Mkoani Mwanza kupitia ufadhili wa Benki hiyo.

Mwakilishi wa  Benki ya Dunia  nchini Dkt.Safari Aquiline amebainisha hayo wakati wa ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa shule ya awali na msingi Shilabela pamoja na shule ya sekondari Mwambola zilizoko wilayani humo.

 

Dkt.Aquiline amesema kuwa ujenzi wa shule hizo uliotekelezwa kupitia mradi wa kuboresha mazingira ya Ujifunzaji na Ufundishaji kwenye shule za awali na Msingi nchini(BOOST) pamoja na mradi wa kuboresha elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP) umefanyika kwa viwango vya ubora na thamani ya shilingi billioni 1.124 zilizotumika  inaonekana.

 

“Nashukuru sana maana ukienda mahali ukakuta Mmama anashika hatamu unafurahi,umeupiga mwingi sana,umeupiga mwingi kwa kusaidiana na mkurugenzi.What you did is the real outcome of what we want to be reflect”alisema Dkt.Aquiline na kuongeza kuwa

 

“Baada ya kuenjoy fleva ya Boost,sasa na enjoy  fleva ya Sequip,kwamba you are sharing the same trend,kile ambacho mmekionyesha kwa upande mwingine na hapa it’s the same.You have dublicated the effrort and outcome ambazo mwisho wa siku naona kwamba kile ambacho kimetoka kinaashiria kwamba kweli kuna thamani ya fedha”  


Mwakilishi wa  Benki ya Dunia  nchini Dkt.Safari Aquiline pia amehimiza utunzaji wa miundombinu ya elimu ili kuwezesha miundombinu hiyo kunufaisha kizazi cha sasa na vijavyo.

 

“Sisi tunapofika na kuona kuna mazingira mazuri mmeyaandaa ambayo yanaonyesha kwamba kile kilichojengwa kimefikia ubora unaostahili Tunawashukuru sana na tunawapongeza na Mimi naomba niwapongeze kwa hilo kwa sababu mmefanya Jitihada nzuri,kile ambacho kimefanyika kinaonekana”alifafanua Dkt.Aquiline


Aidha Benki hiyo imeonesha nia ya kutoa fedha zaidi kwa ajili ya kutatua changamoto ya shule za awali na msingi pamoja na sekondari zilizojengwa kupitia miradi ya Boost na Sequip ikiwemo ukosefu wa nishati ya umeme,maji pamoja na uzio baada ya kutekelezwa kwa ufanisi kwa miradi hiyo iliyohusisha ujenzi wa miundombinu ya elimu.

 

Ushirikiano baina ya viongozi na watendaji wa Halmashauri ya wilaya Misungwi ndio umewezesha miradi ya BOOST na  SEQUIP kutekelezwa kwa viwango vya ubora.

 

“Sina cha kumpa lakini mwenyezi mungu ndo atajua cha kumpa Afisa elimu wetu wa sekondari ambaye alihamia hapa kwa ajili ya kusimamia kwa karibu mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Mwambola,alikuwa kila siku akiamka yuko hapa ndio maana tukafanikisha ujenzi wa shule hii”alisema Clement Matenga mwenyekiti wa  kijiji cha mwambola

 

Wakizungumza wakati wa ziara ya ujumbe wa Benki ya dunia,baadhi ya Jamii zilizonufaika na ujenzi wa shule za Mwambola na Shilabela wameiomba serikali kutatua changamoto zilizosalia ikiwemo ukosefu wa nishati ya umeme,nyumba za walimu,Bweni,Maji pamoja na uzio ili kuimarisha mazingira ya kujifunza na kufundishia.

 

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa elimu ya awali na Msingi ofisi ya Rais Tamisemi Susan Nusu ameiagiza uongozi wa mkoa wa mwanza kuhakikisha kuwa nishati ya umeme na huduma ya maji zinapatikana kwenye shule hizo.

 

“Na sisi tumekuja hapa septemba,naamini kabla mwisho wa mwaka huu wa fedha tutarudi tena kwa ajili ya kuja kujiridhisha mita mia tano je nguzo hata zimesimama,Maelekezo ya serikali ni kwamba Taasisi zote za umma au zozote zinazotoa huduma kwa jamii zipate huduma muhimu kama umeme na maji,hili la umeme Tanesco waongeze kasi mita mia tano sio mbali,tuhakikishe umeme unafika,humu ndani naamini tutakuwa na vifaa vya Tehama muda si mrefu hatutaki walimu wetu wapate shida kwa sababau mazingira tayari yameboreshwa kama yanavyoonekana”alisema Nusu

 

Kuhusu changamoto ya maji katika shule ya sekondari mwambola,Nusu ametaka kutatuliwa kwa changamoto hiyo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu huku akiiasa Jamii ya Mwambola kuibua mradi wa ujenzi wa bweni ili kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu.

 

Kwa upande wake,Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Mkoani Mwanza Chagu Ng’homa ameuhakikishia ujumbe huo kuwa suala la ukosefu wa nishati ya umeme linashughulikiwa na shirika la umeme nchini(Tanesco)na litapatiwa ufumbuzi hivi karibuni huku akiahidi upatikanaji wa maji ya kisima kwenye shule hiyo kabla kumalizika kwa mwezi huu.

 

“Tunatarajia wiki ijayo tuwalete Ruwasa kwasababu Taarifa inaonyesha kuwa maji yapo na yanafaa kwa matumizi ya binadamu,kwa hiyo next week tutapata maji ya kisima hapa kwa sababu maji ya bomba bado yako mbali lakini tutahakikisha maji ya kisima yako hapa”alisema Ng’homa.

 

Mradi wa Boost wilayani Misungwi umehusisha ujenzi wa shule mbili za awali na msingi Shilabela na Mwabebea huku Mradi wa Sequip ukihusisha ujenzi wa shule ya Sekondari Mwambola pamoja na kugharamia ukarabati wa miundombinu ya baadhi ya shule za msingi na sekondari. 


Utekelezaji wa Miradi ya Boost na Sequip wilayani misungwi umegharimu shilingi billioni 3.3 tangu mwaka wa fedha wa 2022/2023








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top