Gonjwa la Kutisha Latua Nchi Jirani

GEORGE MARATO TV
0


Kuripotiwa kwa Mgonjwa wa tatu mwenye maradhi ya Homa ya Nyani Kenya ni hatari kwa nchi Tanzania kama tahadhali haitachukuliwa.

Wizara ya Afya imethibitisha kuwepo mgonjwa wa tatu wa Homa ya Nyani {Mpox} nchini, huku mgonjwa wa kike mwenye umri wa miaka 30 jijini Nairobi akipimwa na kukutwa na maradhi hayo .

Mkurugenzi Mkuu wa Afya Dk.Patrick Amoth amesema kuwa mgonjwa, huyo ambaye ana historia ya kusafiri kuelekea Uganda hivi karibuni , kwa sasa yuko katika hali nzuri na anapatiwa matibabu katika sehemu aliyotengwa katika mji mkuu.

Kisa hiki cha hivi punde kinafanya jumla ya watu waliothibitishwa kuwa na Mpox nchini Kenya kufikia watatu, baada ya wagonjwa wengine kugunduliwa katika kaunti za Taita Taveta na Busia.

Hadi sasa, Wizara imepima jumla ya sampuli 89 za Mpox, huku 79 zikiwa hazina huku saba zikiwa zinaendelea kufanyiwa uchunguzi.


Dkt. Amoth amesisitiza kuwa Wizara imekuwa ikifuatilia kwa karibu hali hiyo na imeongeza kwamba juhudi za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo zinaendelea.

Ufuatiliaji unaoendelea unajumuisha ukaguzi wa wasafiri katika Bandari maalumu za kuingia nchini, na zaidi ya watu 582,000 wamekaguliwa kufikia sasa.

Wizara ya Afya inawataka wananchi kuwa watulivu, ikihakikisha kuwa mfumo wa huduma za afya umejipanga kikamilifu kukabiliana na ugonjwa huo.


“Tunapenda kuwahakikishia wananchi kuwa vituo vyetu vya kutolea huduma za afya vimejiandaa kikamilifu kupima na kudhibiti ugonjwa huu na hakuna haja ya kuwa na hofu Tunaendelea kujitolea kulinda afya na ustawi wa wananchi wote na tutaendelea kukabiliana na maradhi hayo," alisema Dk Amoth.

Hakuna kisa hata kimoja cha ugonjwa huo nchini Tanzania kwa hivi sasa ambacho tayari kimeripotiwa, lakini wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhali kubwa kutokana na mwingiliano mkubwa wa wananchi kwa mataifa haya mawili.

Tayari wizara ya afya nchi Tanzania ilishatataja dalili za ugonjwa huo na kuwataka wananchi wake kuchukua tahadhali kubwa ili kuepuka janga hilo.

               Chanjo ya Vial ya Mpox

Chanzo: Wizara ya Afya Kenya

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top