Aweso Vijana Cup Yazidi Kutimua Vumbi Pangani

GEORGE MARATO TV
0


NA: MWANDISHI WETU, PANGANI

Ligi ya mpira wa miguu inayoratibiwa na Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Pangani ijulikanayo kwa jina la Aweso Vijana Cup, imeendelea kutimua vimbi Aprili 15, 2026, ambapo imezikutanisha timu kutoka Kata za Madanga na Kimang'a, mechi iliyochezwa katika uwanja wa Jaira ndani ya Kata ya Madanga.

Katika mechi hiyo, timu ya Kimang'a ilipata ushindi wa magoli (2-1) dhidi ya Madanga. 

Mratibu wa mashindano hayo, Ramadhani Kibendera amesema mashindano hayo yameleta mwamko mkubwa kwa vijana kushiriki katika michezo kwani michezo ni fursa ya kujenga na kukuza mahusiano, kipaji na ajira. 

"Mwamko wa vijana kushiriki mashindano haya ni mkubwa, timu zinatoa upinzani mkali, na tunatarajia vijana wengi kupata fursa kupitia mashindano hayo," amesema Kibendera.



Sambamba na hilo, Kibendera amesema mdhamini wa mashindano hayo, Mbunge wa Pangani na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, anatimiza jukumu lake la kutoa mahitaji yote muhimu ya kufanikisha uendeshaji wa mashindano hayo.

Hii ni mechi ya sita tangu kuanza kwa mashindano ya Aweso Vijana Cup yaliyozinduliwa Aprili 4, 2026, na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Musa Mwakitinya. 





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top