Serikali Kukusanya Takwiku za Sekta Isiyo Rasmi Ili Zichangie Uchumi wa Taifa

GEORGE MARATO TV
0

 DODOMA.

‎SERIKALI kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetangaza kuanza kwa tafiti mbalimbali za kitaifa zitakazolenga kukusanya taarifa za kina kuhusu shughuli za kibiashara, sekta isiyo rasmi pamoja na uzalishaji viwandani ili kusaidia kuboresha mipango ya maendeleo ya uchumi nchini.

‎Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Amina Msengwa amesema utekelezaji wa tafiti hizo unafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Sura ya 351 ambayo inaipa NBS jukumu la kuratibu na kusimamia uzalishaji wa takwimu rasmi nchini.

‎Amesema tafiti hizo ni pamoja na Utafiti wa Kina wa Shughuli za Kibiashara, Utafiti wa Sekta Isiyo Rasmi, Utafiti wa Huduma za Fedha kwa Wafanyabiashara Wadogo Sana, Wadogo na wa Kati (Finscope MSMEs) pamoja na Utafiti wa Uzalishaji Viwandani.

‎Kwa mujibu wa Dkt. Msengwa, tafiti hizo zinalenga kukusanya taarifa muhimu kuhusu uzalishaji viwandani, ajira, uwekezaji na mazingira ya biashara ili kusaidia kubaini mwenendo wa ukuaji wa biashara na viwanda nchini.

‎“Madhumuni ya tafiti hizi ni kukusanya taarifa muhimu kuhusu shughuli za biashara katika sekta rasmi na zisizo rasmi, zitakazosaidia Serikali na wadau mbalimbali kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini,” alisema.

‎Aidha, alieleza kuwa kupitia utafiti wa Huduma za Fedha kwa Wafanyabiashara (Finscope MSMEs), Serikali itapata takwimu muhimu zitakazosaidia kupima maendeleo ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Ujumuishaji wa Kifedha Awamu ya Tatu pamoja na Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha.

‎Kwa upande wa utafiti wa uzalishaji viwandani, alisema utawezesha kupatikana kwa taarifa muhimu ikiwemo idadi ya viwanda, aina ya bidhaa zinazozalishwa, idadi ya wafanyakazi, gharama za uzalishaji pamoja na mapato yatokanayo na uzalishaji.

‎“Taarifa zitakazopatikana kupitia tafiti hizi zitaisaidia Serikali kupanga sera na mikakati madhubuti ya kuimarisha sekta ya biashara na viwanda pamoja na DODOMA.

‎“Taarifa zitakazopatikana kupitia tafiti hizi zitaisaidia Serikali kupanga sera na mikakati madhubuti ya kuimarisha sekta ya biashara na viwanda pamoja na kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa,” aliongeza.

‎Zoezi la ukusanyaji wa taarifa linatarajiwa kufanyika kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia Machi 11 hadi Mei 10, 2026, likihusisha wadadisi 713 na wasimamizi 69 watakaotembelea kaya, biashara na viwanda katika maeneo mbalimbali nchini kukusanya taarifa kwa kutumia teknolojia ya vishikwambi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top