Mkuu huyo wa wilaya ya Serengeti ametoa kauli hiyo wakati wa neno kwa waumini wa dini ya Kislamu walioshiriki kwenye futari iliyoandaliwa na taasisi ya Nyansaho foundation.
Amesema hivi karibuni kumezuka mtindo wa baadhi ya watu kutotofuata misingi ya Sheria badala yake wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi jambo ambalo ni kinyume cha sheria na linakiuka maagizo ya mwenyezi Mungu.
"Nalaani vikali kitendo kilichofanyika hivi karibuni katika kijiji Cha Nyechoka ambapo umefanyika uvamizi na watu kubomolewa nyumba zao'alisema DC Angelina
Aidha mkuu huyo wa wilaya ya Serengeti ameipongeza Taasisi ya Nyansaho foundation kwa kuandaa futari hiyo ambayo amesema imewaleta pamoja waumini wa dini ya Kislamu na dini nyingine wilayani Serengeti,jambo ambalo amesema linalenga kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao.
"Taasisi hii ya Nyansaho foundation imekuwa ikitoa huduma za Elimu Afya na mahitaji maalumu Kwa wananchi katika mkoa wa Mara, lakini sasa katika mwezi huu mtukufu imeweza kuwafikia waumini wa dini ya Kislamu kwa wilaya yetu ya Serengeti na wilaya nyingine za mkoa wa Mara kufanya tendo hili jema kwa mwenyezi Mungu.
Naye Msemaji wa Taasisi hiyo ya Nyansaho foundation Bi Modesta Mwema ambaye pia ni mtaribu wa taasisi hiyo, amesema mkakati wa taasisi hiyo ni kumfikia Kila mhitaji katika nchi nzima ya Tanzania.
Amesema Taasisi ya Nyansaho foundation ni taasisi isiyo ya kiserikali yenye malengo ya kusaidiana na Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali ndani ya jamii na kwamba milango ipo wazi kwa kila mdau katika kushirikiana ili kuinua maisha ya mwananchi.
Naye sheikh wa wilaya ya Serengeti Juma Abdallah, ameipongeza taasisi hiyo ya nyansaho foundation na kusema imekuwa ya mfano Bora katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan Kwa kujitoa kwenye jamii hususani katika wilaya ya Serengeti, huku pia akiwataka wananchi kuwa na uvumilivu na kutokuwa na moyo wa kulipa visasi pale panapokuwapo na changamoto.











